Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Hashim A. Komba amezindua kampeni ya utoaji wa chanjo ya Polio leo Septemba 2022 kwa watoto wenye umri chini ya Miaka Mitano katika ZAHANATI YA Namatumbusi kata ya Nang'ondo, ambayo itatolewa kwa muda wa Siku Nnne kuanzia leo Septemba 1 hadi 4 2022 . Chanjo hii ni ya awamu ya pili kwa wilaya ya Nachingwea na ya Tatu Kitaifa . Hivyo kwa watoto wote waliopata Chanjo awamu ya kwanza wanapaswa kupata tena kwa lengo la kuimarisha kinga hiyo na wale ambao hawakupata wanastahili kupata kwa awamu ya kwanza.
Aidha, Mhe. Komba amewataka wakazi wa wilaya ya Nachingwea kupuuza baadhi ya maneno ya wachahce yanayolenga kupotosha chanjo hiyo, kwani lengo la Serikali ni kulinda watoto na si vinginevyo.
Aewasihi wazazi, walezi na ndugu na jamaa kuwahamasisha wale wote wenye watoto wenye umri chini ya maiaka mitano kuhakikisha wanapata chanjo hiyo muhimu. Chanjo hiyo itatolewa na wataalum wa Afya Nyumba kwa Nyumba na katika vituo vyote vya kutolea huduma ya Afya ndani ya Wilaya yote ya Nachingwea.
Ikumbukwe zoezi ili ni la kitaifa linaendelea kote nchini Tanzania .
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.