Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa wilaya ya Nachingwea Mhe. Hashim_komba ametangaza tarehe rasmi ya usaili wa kazi ya muda Sensa ya watu na Makazi ya Agosti 23, 2022 kuwa ni tarehe 22/07/2022 katika kila kata ndani ya wilaya ya Nachingwea.
Mhe. Komba amewatahadharisha kamati za kata kutojihusisha na taratibu zozote zitakazoenda kinyume na maadili ya kazi ikiwemo kupokea rushwa katika zoezi la usaili.
Wahusika wote ambao wamepata nafasi ya kushiriki Sensa watafanyiwa usaili katika kata zao ambazo wameomba.
Aidha, Mhe. Komba amewasisitiza viongozi wote ndani ya wilaya kuendelea kuhamasisha na kutoa Elimu kwa Umma juu ya umuhimu wa Sensa ya watu na Makazi.
@nbs.tanzania
.#kaziinaendelea
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.