Tarehe 1 Agosti 2025 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala, akiwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini, amekagua banda la Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea lililopo katika viwanja vya Ngongo, Lindi.
Akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mhe. Mohamed Hassan Moyo, Kanali Sawala alipata fursa ya kujionea utekelezaji wa miradi ya maendeleo, huduma za kijamii na fursa za kiuchumi zinazotolewa na Halmashauri hiyo kwa wananchi.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni:
"Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025."
Maonesho haya yanaendelea kuvutia taasisi mbalimbali, huku Halmashauri ya Nachingwea ikiendelea kutoa elimu na huduma kwa wananchi kupitia banda lake.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.