Mkuu wa Divisheni Elimu Msingi Mwalimu Stephen Urassa wa Halmashauri ya Nachingwea ameziomba jamii kushirikiana na walimu kuhakikisha watoto wa darasa la awali, darasa la kwanza pamoja na madarasa mengine wanaripoti shuleni kwa wakati ili waweze kuendelea na ratiba za masomo. Hayo ameyasema January 8, 2024 alipokua Shule ya Msingi Stesheni katika zoezi la ufuatiliaji wa uripoti wa wanafunzi.
Ndugu Urassa ametoa pongezi kwa Shule ya Msingi Stesheni pamoja na Wazazi katika shule hiyo kwa kuweza kuzidisha 50% ya wanafunzi katika siku ya kwanza ya kufunga shule. Hali ya uripoti inaridhisha katika shule mbalimbali za msingi kwani Wazazi wameitikia vizuri katika kuwaandikiasha watoto katika darasa la awali na darasa la kwanza.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.