.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo amezitaka taasisi za umma na Halmashauri ya Nachingwea kushirikiana katika kuhakikisha miradi inakamilika kwa kuzingatia kanuni zote na taratibu zilizowekwa, hayo ameyasema leo Oktoba 8, 2024 alipokua katika kikao cha kutoa Elimu kuhusu miradi.
Katika kikao hicho ambacho kimehusisha Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Nachingwea, Takukuru, Polisi, TRA na Waheshimiwa madiwani ambao katika kata zao wamepokea miradi ya SEQUIP na BOOST 2024, mheshimiwa Moyo amesisitiza upatikanaji wa nyaraka katika kila hatua ya mradi ili kuhakikisha mpaka mradi unapokamilika basi nyaraka zote zinakuwepo.
Sambamba na hilo amemuagiza Mwanasheria wa Halmashauri kuandaa Mkataba utkaowaongoza wasimamizi wa miradi kukusanya nyaraka zote muhimu, pia ametoa rai kwa maafisa wa Manunuzi kuandaliwe utaratibu wa kuwa na bei elekezi za vifaa vya ujenzi ili kuwaongoza wasimamizi na kuepuka matumizi mabaya ya fefha za umma.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nachingwea Mheshimiwa Mohamed Hassan Chiwalo alisisitiza suala la kuzingatia taratibu za manunuzi na ujenzi, pia amewataka viongozi kushirikisha jamii katika utekelezaji wa miradi.
Aidha, Afisa wa Takukuru ndugu Mafulu Aloyce ametoa elimu na kusisitiza kuwa na utaratibu wa kufuatalia kwa karibu utekelezaji wa miradi na kuzingatia matumizi ya Vitabu vya saiti na vitabu vya kutunzia kumbukumbu.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.