Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Mhandisi Chionda Kawawa, ametoa wito kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu vilivyonufaika na mkopo wa asilimia 10 ya mapato ya halmashauri, kuhakikisha wanatumia mikopo hiyo kwa uaminifu na uwajibikaji mkubwa.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi mikopo hiyo yenye thamani zaidi ya shillingi millioni 649,
Mhandisi Chionda, amesema kuwa fedha hizo zimetolewa ili kuongeza fursa za kiuchumi kwa vikundi 54 vilivyokidhi vigezo ili kusaidia kupunguza umasikini katika jamii,
Amesisitiza kuwa uaminifu na nidhamu ya matumizi ya mikopo hiyo ni nguzo itakayosaidia vikundi vingi zaidi kunufaika na mpango huo katika siku zijazo lakini pia itawaepusha kuingia katika mikopo yenye riba kubwa na isiyokua na tija katika maendeleo yao,
"Tunawaomba muwe waaminifu katika kuzitumia fedha hizi. Lengo letu ni kuona vikundi vikikua na kuchangia maendeleo ya kiuchumi ya wilaya yetu,”
Aidha, Mkurugenzi amezitaka kamati zinazohusika na usimamizi wa mikopo hiyo kuhakikisha kuwa fedha hizo zinarudi kwa wakati ili vikundi vingine viweze kunufaika na fursa hii.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.