Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Mheshimiwa Jumanne Abdalah Sagin ametoa pongezi na Shukrani kwa Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea wananchi kampeni ya Kitaifa Msaada ya Kisheria, hayo ameyasema leo february 19, 2025 alipokua katika Uzinduzi wa Kampeni hiyo uliofanyika Wilayani Ruangwa.
Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais na wadau mbalimbali inatekeleza kampeni ya Mama Samia na tayari imeshatelezwa katika mikoa 17 na katima mwezi February inatekelezwa katika mikoa 5 ambako ilianza Mwanza, Lindi, Mbeya, Rukwa na Pwani
Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imekua na matokeo chanya kana kuongezeka kwa uelewa wa kisheria katika nyanja mbalimbali kama jinsia na watoto, utawala bora, haki za binadamu na elimu ya uraia.
Aidha, Wizara imeendelea kuwajengea uwezo watoa msaada kisheria ili kuendelea kuwaletea huduma za kisheria wananchi na mara baada ya uzinduzi huduma hii itatolewa kuanzia February 20 hadi 28 katika kata kumi na vijiji au mitaa 3 kwa kila halmashauri na ikumbukwe huduma hizi zinatolewa bure kwa wananchi wote ili wafahamu wajibu na haki zao.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.