Leo, tarehe 4 Aprili 2025, Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mheshimiwa Dkt. Amandus Chinguile, akiambatana na Kamati ya Mfuko wa Jimbo, ametembelea Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea na kutoa jumla ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya kumalizia ukarabati wa Wodi Namba 3, baada ya awali kutoa milioni 10. Ukarabati huu unatarajiwa kugharimu jumla ya milioni 35,382,600.
Mheshimiwa Dkt. Chinguile amekagua pia ujenzi wa uzio wa Shule ya Nachingwea Girls, ambao fedha za Mfuko wa Jimbo umetoa shilingi milioni 17 kuchangia ujenzi wa uzio huo.
Ameweka jiwe la msingi kwenye shule mpya za sekondari katika Kata ya Nachingwea na Mtua, na pia ametembelea ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Kipara Mtua, ambapo Mfuko wa Jimbo umechangia zaidi ya shilingi milioni 6,500,000.
Wananchi wamemshukuru Mheshimiwa Mbunge na Kamati ya Mfuko wa Jimbo kwa kuboresha huduma za afya, elimu, na miundombinu, huku wakieleza manufaa makubwa ya miradi hiyo katika kata zao.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.