Leo, tarehe 8 Machi 2025, maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yamefanyika kimkoa wilayani Nachingwea, mkoani Lindi, katika viwanja vya Maegesho ya Malori. Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, ambaye alikuwapo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Katika hotuba yake, Mheshimiwa Moyo aliwakumbusha wazazi na walezi kuhusu umuhimu wa kuhakikisha watoto wanakua salama, akieleza kuwa jumla ya watoto 7,840 wamepata mimba. Amessiitiza jukumu la jamii katika kulinda mustakabali wa watoto, hasa wasichana, ili kuwaepusha na changamoto za kimaisha.
Aidha, Mheshimiwa Moyo amewahimiza wanawake kuchangamkia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa vikundi vya wanawake, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 1.8 kimepangwa kugawiwa kwa vikundi 435 vyenye wanufaika 2,175. Aliwaomba wanawake kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili kunufaisha wananchi wengine.
Pia, Mheshimiwa Raisi alitoa fursa kwa wanawake kugombea nafasi za udiwani na ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, akisisitiza umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika uongozi na maamuzi ya kitaifa.
Hafla hiyo ilijumuisha vikundi mbalimbali vya wanawake, wadau wa maendeleo, na viongozi wa jamii, ikiwa ni ishara ya kuenzi mchango wa wanawake katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.