Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt Hussen Mwinyi amesema mgogoro kati ya wananchi na vikosi vya 41 KJ na 843 KJ utatuliwa hivi karibuni.
Dkt Mwinyi ameyasema hayo jana kwa nyakati tofauti alipoongea na wananchi hao katika katika vijiji vya Kilimanihewa na Mkukwe alipokwenda kujionea hali halisi ya mgogoro huo.
Amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati wizara yake ikipitia nyaraka mbalimbali ambazo zitasaidia kutatua mgogoro huo ikiwemo ripoti ya kamishna wa Ardhi kanda, Brigedia Jenerali Mwangole na tume ya Mkuu wa Mkoa.
“Nimesikiliza upande wa Jeshi na upande wenu wananchi kitachatakiwa hapa ni kila anayestahili kupata haki apate haki yake, naomba mnipe muda nikapitie ripoti mbalimbali zilizotajwa ili mimi na wenzangu Serikalini tuweze kutoa maamuzi ya haki” Alisema Dkt Mwinyi
Mapema akielezea mgogoro huo Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Mheshimiwa Hassan Masala amesema ni shauku yake mgogoro huo upate ufumbuzi mapema kwa maslahi ya wananchi na jeshi
Aidha katika taarifa yao kwa Waziri huyo, walisema hawaruhusiwi kuingia katika maeneo hayo ambayo yana mikorosho waliyoihudumia lakini wamezuiwa kuvuna korosho hizo.
Dkt Mwinyi amewataka wakulima kutoingia katika maeneo hayo mpaka pale mgogoro huo utakapokwisha, na pia ameagiza korosho zote zilizovunwa katika maeneo hayo malipo yake yasitishwe mpaka pale ufumbuzi utakapopatikana.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.