Shirika la LIWOPAC kwa kushirikiana na SATF wametoa msaada wa baisikeli mbili za mataili matatu kwa wanafunzi wawili wenye ulemavu wa miguu Wilayani Nachingwea, wanafunzi hao ni Baraka Ali Saidi wa Kidato cha pili katika Sekondari ya Wavulana ya Rugwa na wa kidato cha tano kutoka shule ya sekondari ya Pugu iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Hayo yamefanyika leo Julai 25, 2025 katima ofisi ya Mkurugenzi Mtwndaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea.
Akizungumza kwa niaba ya shirika la LIWOPAC bi Nyama amesema, shirika hilo kwa kushirikiana na SATF wanafadhili jumla ya wanafunzi 52 wenye mazingira magumu katika Wilaya ya Nachingwea na kwa siku ya leo wametoa baisikeli hizo mbili kama sehemu ya misaada ambayo wamekua wakiitoa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda Kawawa ametoa shukrani zake kwa mashirik hayo na kuwapongeza kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kuondoa umasikini kwa jamii za watanzania na kuahidi kutoa ushirikiano na kuunga mkono jitihada wanazozifanya.
Aidha, mmoja wa wanafunzi hao aliyefahamika kwa jina la Baraka Ali Saidi ametoa shukrani zake kwa LIWOPAC na SATF na kuwaomba kuendeleza misaada hiyo kwa watu wenye uhitaji, pia ameta ahadi ya kuhakikisha anazingatia masomo ili kufikia.malengo yake.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.