Katibu tawala wilaya ya Nachingwia ndugu Haji Mbaluku kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ameshiriki maafali ya kwanza ya darasa la saba ya shule ya Msingi Muzdalifa iliyopo Kata ya Nachingwea yaliyofanyika Agosti 31, 2024 shuleni hapo.
Katika sherehe hizo wahitimu 38 ambao kati yao18 ni wavulana na 20 ni wasichana, pia sherehe hizo ziliambatana na harambee cha kuchangia maboresho ya shule, mdugu Mbaluku ametoa Shilingi 500,000 kutoka kwa Mkuu wa wilaya ili kuiunga mkono shule ya hiyo.
Das Mbaluku amewasihi walimu, wazazi na wadau mbalimbali wa Elimu kutoa ushirikiano ili kuunga mkono jitihada za shule hiyo kwani haina chanzo kingine cha mapato zaidi ya ada, shule inafanya vizuri kitaaluma watoto wengi wamekwenda shule maalum wakitokea katika shule hiyo.
Aidha kwa upande wake ndugu Ahmad Said Liyuu Mkurugenzi wa shule ya Muzdalifa amewashukuru wazazi kwa mchango wao mkubwa katika maendeleo ya shule hiyo na amewataka kuendelea kuwashika mkono.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.