Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Abubakari Kunembe ametoa Shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kuleta utatuzi wa kero na changamoto mbalimbali za wananchi kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia,
Hayo ameyasema leo February 19, 2025 alipokua katika Uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Wilayani Ruangwa.
Mheshimiwa Kunembe amesema Kampeni hii inawagusa moja kwa moja na kuwasaidia Watanzania wa kawaida wanaokutana na changamoto katika masuala mbalimbali na hawana uwezo wa kujipatia huduma za kisheria, hivyo ni jambo kubwa na linawainua wananchi.
Pia, ametoa shukrani kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukubali kushiriki na kua mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hii pamoja na kua majukumu mengi, kwani kwa Mkoa wa Lindi katika kila wilaya kumewekwa wasaidizi wa kisheria kwa ajili ya kutoa huduma hii ya misaada ya kisheria ili kufikisha huduma kwa wananchi wa chini.
Aidha, amempongeza Rais Dokta Samia Suluhu Hassan pamoja na kuanzisha kampeni ya Mama Samia lakini pia ametoa fedha zaidi ya trioni 1.32 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo katika Mkoa wa Lindi.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.