Kmati ya Fedha , Uongozi na Mipango ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Adinan Mpyagila akiambatana na makamu mwenyekiti Mhe. Veronica Makotha sambamba na wataalamu na waheshimiwa madiwani ambao ni wajumbe wa kamati hiyo, Oktoba 17, 2022 imetembelea vyanzo mbalimbali vya mapato kwa lengo la kuona namna vyanzo hivyo vinavyofanya kazi zake na kubaini ubora ama changamoto zake kwa lengo la kuboresha zaidi,
Baadhi ya vyanzo vilivyotembelewa ni vyoo vya soko kuu Stendi ya zamani na Stendi mpya, Utendeji wa Soko la voda, Soko la Tundulu ya leo, maegesho yamalori, Nyumba za kulala wageni na kitegeuchumi cha Halmashauri, Machimbo ya madini ya ujenzi, .
Ziara hii inaendelea mara kwa mara kwa lengo la kuhakikisha halmashauri inapata mapato yake ipasavyo.
baadhi ya picha ya vyanzo hivyo
Mgogi wa madini ya ujenzi kata ya Nangowe
Soko la Voda
Machimbo ya mchanga kwa ajili ya ujenzi
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.