Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea imepongezwa kwa usimamizi wa matumizi sahihi wa mapato ya ndani ya Halmashauri yanayotokana na ushuru na tozo mbalimbali hasa mazao ya biashara ikiwemo korosho , ufuta na mbaazi .Pongezi hizo zimetolewa na Katibu wa UWT Taifa Bi. Phili Nyambi alipofanya ziara kata Mbondo Wilayani Nachingwea .Katibu ametoa pongezi hizo alipotembelea kituo Cha Afya kilichojengwa kata ya Mbondo kilichotengewa Milioni 400 kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ambazo zimejenga maabara, Jengo la kufulia na OPD na tayari kituo hicho kimeanza kazi Mara baada ya kupelekewa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 100 . Ziara hiyo amefanyika Wilayani Nachingwea ikiongozwa na mwenyekiti wa jumuiya hiyo (UWT ) Bi. Marry Chatanda na wajumbe wa kamati ya utekelezaji Taifa ambao wakagua miradi mwingine ndani ya wilaya .Katibu licha ya kukagua miradi kadhaa kata ya mbondo aliweza kufanya Mkutano wa hadhara na kuzungumza na wananchi namna serikali inavyofanyakazi ya kuwatumikia wananchi. #tukovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.