Timu ya FORLAND ikiongozwa na Ndugu. Michael Hawkes ambaye ni mshauri Mkuu wa mradi imetembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Nachingwea na kukutana na Timu ya wataalamu wa Halmashauri ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi ndugu Joshua Mnyangali kwa ajili ya kuutambulisha rasmi mradi wa usimamizi endelevu wa misitu na ardhi,
Utambulisho wa mradi huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri Julai 22, 2025.
Akiutambulisha mradi huo Ndugu. Michael Hawkes amesema ,mradi unalenga kuimarisha maisha ya wananchi kupitia matumizi bora ya ardhi na rasilimali za misitu kwa njia shirikishi.
Aidha, kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo amewataka Viongozi wa Vijiji 12 vitakavyonufaika na mradi watoe ushirikiano ili thamani halisi ya mradi huu iweze kuonekana.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.