Leo, tarehe 3 Machi, Taasisi ya Essence of Smile Foundation, kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Jamii wamekabidhi vifaa vya shule kwa watoto watano wenye uhitaji kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe.Mohamed Hassan Moyo.
Mhe.Moyo amewapongeza kwa kujitolea kwao kusaidia watoto kupata vifaa vya shule, jambo linaloathiri sana maendeleo ya masomo ya vijana wetu. Amesitiza kuwa hata vitabu vya Mungu vinatufundisha kutoa.
Taasisi ya Essence of Smile Foundation, kupitia msemaji wake Paul Leonald Anga, pamoja na Queenrose Kifumu (Muhazini), wamemwakilisha Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Nubtse Isack Abeli.
Katika mpango wao, wameanza na wanafunzi watano, lakini lengo lao ni kuwafikia zaidi ya hao, licha ya changamoto ya rasilimali.
Wanapenda kuunga mkono juhudi za Mhe. Raisi katika kuboresha sekta ya elimu, akitumia fedha nyingi kuleta mabadiliko. Kwa mwaka ujao, wanatarajia kugusa wanafunzi wengi zaidi na wameomba kuungwa mkono kutoka kwa wadau ili kufanikisha lengo lao la kuwasaidia watoto wengi zaidi.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.