Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wa Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda A. Kawawa amewapongeza sana wanawake wapenda maendeleo kwa wazo lao kubwa lenye tija kwa wakazi wa Nanachingwea. Mhandisi Kawawa amesema wiki hii inatoa tafakuri ya kufikiria makundi mbalimbali na wanawake wamekua mstari wa mbele kumkomboa mwanamke katika kujiinua kiuchumi.
Mhandisi Chionda ametoa rai kwa wanaume wa Nachingwea kuguswa na kushiriki katika kuyafikia makundi mbalimbali. Aidha, katika harambee hiyo Mhandisi Chionda amechangia kiasi cha fedha Sh1,000,000/= pamoja na chakula kwa wahanga hao.
Pia, Mkurugenzi Mtendaji amewakumbusha wanawake na wadau mbalimbali wa maendeleo juu ya kuendelea na kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia na Kusisitiza jamii umuhimu wa elimu ya Utunzaji na uhifadhi wa mazingira na Wanawake kutimiza majukumu ya malezi.
Aidha, kwa upande wa Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Nachingwea ndugu Veronica Makota ametilia mkazo juu ya umuhimu kujitoa katika kuwasaidia wakazi wa kata za Ngunichile na Nditi na maeneo mengine yaliyoathiriwa na Tembo, amesema hali ya kata hizo mbili ni mbaya wananchi wanategemea kula upupu na Angadi (Mizizi pori yenye sumu), hivyo amewasihi wadau mbalimbali kukuguswa na kuwasaidia. Pia, amewasisitiza wanawake kugombea kuingia kwenye nafasi za maamuzi katika uchaguzi huu serikali za mitaa
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.