Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Mhandisi Chionda Kawawa, ametoa wito kwa wananchi wote kutembelea banda la Nachingwea katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika Ngongo Mkoani Lindi,
Chionda amesema banda hilo limeandaliwa kwa lengo la kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na halmashauri ikiwa ni Kilimo, Uvuvi mifugo, ujasiriamali pamoja na elimu kuhusu madini ambayo yanayopatikana katika wilaya ya Nachingwea
Aidha, Mkurugenzi amebainisha kuwa kupitia banda hilo wananchi watapata nafasi ya kuuliza maswali, kupata ufafanuzi na kutoa maoni yao juu ya kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi.
Amehimiza wakazi wa Nachingwea na wageni wengine kutumia fursa hiyo kujifunza na kushirikiana katika kuleta maendeleo, ikiwa kauli mbiu ya mwaka 2025 ni CHAGUA VIONGOZI BORA KWA MAENDELEO YA KILIMO MIFUGO NA UVUVI.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.