Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mh. Mohamed Hassan Moyo, akishirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mh. Goodluck Mlinga, wameufunga rasmi Mgodi wa Mto Mbwemkuru Kiegei, unaomilikiwa na Kampuni ya KAIYUE kwa tuhuma za kutumia zebaki kinyume cha sheria na kufunga mto.
Wakuu hao walisema mgodi huo umeendesha shughuli bila kuzingatia miongozo ya Wizara ya Madini, hivyo umefungwa hadi utakapokidhi masharti ya kisheria. Kaimu Afisa Madini Mkazi, Mhandisi Jackson Simbaufoo, alithibitisha ukiukwaji huo na kusema kuwa hatua hiyo imelenga kulinda rasilimali za taifa, mazingira na kuzuia madhara yanayotokana na kufungwa kwa maji.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.