Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe. Mohamed Hassan Moyo, amewahimiza wananchi kuipa kipaumbele amani na mshikamano, akisisitiza kuwa hatavumilia mtu yeyote atakayevunja utulivu kwa sababu za siasa au kuharibu mali za wananchi na serikali.
“Tubishane kwa hoja na sera, si kuhatarisha amani, usalama na mshikamano wa kijiji chetu au wilaya yetu. Tuwapime wale wanakuja,” amesema.
Amesema hayo Ijumaa tarehe 25 Julai 2025 alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika kata ya Chiumbati, Shuleni, Stesheni na Nangowe, akizungumza na wananchi na kusikiliza kero zao.
DC Moyo amesisitiza kuwa amani ni kipaumbele cha maendeleo na ni msingi wa mafanikio katika kila jamii.
Ziara hiyo inaendelea tarehe 28 Julai 2025 katika Kata ya Mkoka na Kata ya Marambo.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.