MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amewataka maafisa kilimo kutoa elimu kwa wakulima namna bora ya kulima kilimo cha kisasa kama ambavyo wanavyotoa elimu hiyo kwenye nane nane.
Moyo alisema kuwa ukienda kwenye maonyesho ya nane nane unakutana na mazao yamepimwa vizuri kwa viwango vinavyotakiwa lakini ukienda kwa wakulima vijijini hali ni tofauti.
Alisema kuwa Rais Dkt Samia Suhulu Hassan ametoa pikipiki kwa kila afisa kilimo Tanzania hivyo pikipiki hizo zitumike kwenda kutoa elimu kwa wakulima huko vijijini.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.