June 2, 2023 wilayani Nachingwea shughuli za maadhimisho ya miaka 60 ya JKT zilianzishwa na kutamatika leo July 7,2023 katika viwanja vya stendi ndogo ya mabasi yaendayo Liwale huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe Mohamed Hassan Moyo. Mh Moyo amewashukuru Jeshi la Kujenga Taifa kwa kumualika kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo za Kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi hilo na amewapongeza kwa kutimiza miaka 60.
Mhe Moyo amesema taifa limenufaika kupitia Jeshi la Kujenga Taifa na limekua sehemu muhimu ya kufundisha na kuandaa vijana katika utii, uadilifu, uzalendo, ukakamavu pamoja na kufanya kazi kwa bidii na kuipenda nchi yao. Kwa upande wake Mkuu wa vyombo vya Usalama wilaya ya Nachingwea Kanali Sylvesta Ndayahundya Kipeya amesema katika shughuli hizo kama jeshi lilifanya shughuli za kijamii kama vile kufanya usafi Hospitali ya wilaya, Uchangiaji damu pamoja na ujenzi wa banda la kupumzikia abiria chenye thamani ya Sh 4,790,000/= katika stendi ndogo ya mabasi yaendayo Liwale (Maegesho ya Malori).
Aidha, wananchi mbalimbali waliojitokeza katika sherehe hizo wamelipongeza Jeshi la kujenga Taifa na Serikali kwa kufanikisha ujenzi wabanda la kupumzikia abiria katika stendi ndogo ya mabasi yaendayo Liwale na kuomba liongwezwe linguine sambamba na vyoo.
Sherehe hizi za maadhimisho kitaifa zitafanyika Makao makuu ya nchi Mkoani Dodoma ambako yalianza June 3, 2023 na yatamatika July 10, 2023 katika Viwanja vya Jamhuri Dodoma huku Mgeni rasmi atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassani.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.