Tarehe 24 Julai 2025, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe. Mohamed Hassan Moyo, ameanza ziara ya siku nne katika Kata za Naipingo na Mtua kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kukagua miradi ya maendeleo.
Wananchi wa Kata ya Mtua, Wilaya ya Nachingwea, wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwapatia zaidi ya milioni 560 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari, hatua iliyowawezesha wanafunzi kuanza masomo na kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu. Vilevile, zaidi ya milioni 131 zimetolewa kwa ajili ya uboreshaji wa shule ya msingi, sambamba na milioni 40 kwa umaliziaji wa madarasa.
Ziara hiyo imeanzia Kata ya Naipingo, Kijiji cha Kihuwe, na Kata ya Mtua, Kijiji cha Mtua, akiwa ameambatana na wataalamu na kamati ya ulinzi na usalama.
Aidha, Mhe. Moyo amewataka wananchi wa Kata ya Mtua kushirikiana kwa kutoa nguvu kazi katika ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi ili ukamilike kabla ya mvua kuanza, huku akisisitiza usimamizi makini wa miradi hiyo. Vilevile, amewataka wananchi wa Nachingwea kuendelea kumpa Rais Samia kura za kishindo kutokana na kazi kubwa anayofanya ya kuleta miradi ya maendeleo.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.