Julai 29, 2024 Mkuu wa Wilaya ha Nachingwea Mheshimwa Mohamed Hassan Moyo amefanya kongamano kubwa lililo shirikisha viongozi mbalimbali pamoja na wananchi katika ukumbi wa Chuo cha Walimu Nachingwea kwa ajili ya kukusanya maoni ya maadalizi ya dira ya maendeleo ya taifa 2050.
Katika kongamano hilo majadiliano yamefanyika na kuonyesha mafanikio mbalimbali yaliyofanyika katika utekelezaji wa dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2025, mafanikio mbalimbali yamepatikana katika dira hiyo
katika wilaya ya nachingwea, kwa mfano katika sekta ya Afya Mheshimiwa Moyo ameeleza miaka 20 iliyopta
Halmashauri ya Nachingwea ilikua na kituo kimoja cha afya lakini sasa kuna vituo tano vya afya vya kisasa.
Pia, kumekua na mafanikio katika uboreshaji wa miundombinu mbalimbali, ulinzi na usalama na kuongezeka kwa uzalishaji katika kilimo, miaka 20 iliyopita miundo mbinu kama barabara katika Wilaya ya Nachingwea ilikua duni ukilinganisha na sasa, katika Elimu kwa Wilaya ya Nachingwea ina Shule za Msingi zaidi ya 115 ukilinganisha na miaka 20 iliyopita hivyohivyo katika Elimu sekondari shule nyingi na za kisasa zimejengwa.
Wadau na wananchi mbalimbali walioshiriki kongamano hilo wametoa maoni yao kwa ajili ya maandalizi ya dira ya maenedeleo ya 2050, maoni kama uboreshwaji zaodi katika Sekta ya Elimu hususani Elimu bure, Miundo mbinu hasa ya usafirishaji na umeme, uboreshaji zaidi katika sekta ya afya, utwala, ulinzi na usalama bora na maeneo mengine.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda A. Kawawa amewasihi wananchi na wadau mbalimbali kuchangia maoni yao kwani dira 2050 ya maendeleo ndio itakayoeleza namna maendeleo ya taifa yatakavyopatikana kuelekea 2050.
Aidha, Mhe Moyo amewakumbusha na kuwasihi wananchi kuhakikisha wanashiriki katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura na kushirikk katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, kwani viongozi watakaochaguliwa ndio watakaoanza utekelezaji wa dira ya maendeleo ya 2050.
@samia_suluhu_hassan
@ofisi_ya_makamu_wa_rais
@ortamisemi @msemajimkuuwaserikali
@maelezonews
@wizarahmth
@wizara_elimutanzania
@wizara_afyatz
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.