Leo, tarehe 26 March Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo, amegawa mitungi ya gesi 1600 kwa wakina mama waliolipia nusu ya gharama, yaani shilingi 19,500 kila mmoja.
Mheshimiwa Moyo amemshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujitolea kulipa nusu ya gharama za mitungi hii na kuwahakikisha wakina mama wanatumia nishati salama, kuepuka madhara yanayotokana na kuni na mkaa.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kufanya tathmini ya matumizi ya gesi ili gesi inapoisha ili uweze kujaza tena badala ya kufungia mitungi ndani, na kuanza kutumia nishati zisizofaa pia aliwahakikishia wanawake wote waliolipia mitungi kuwa zoezi litaendelea, na mitungi zaidi itapatikana.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.