Kabila la Wamwela kutoka wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi likiongozwa na kiongozi wa Kabila hilo Chifu Ismail Malibiche Nakotyo leo Septemba 18, 2025 limefanya ibada maalum ya kuombea taifa amani kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba mwaka huu.
Akizungumza wakati wa ibada hiyo ya maombi, Kiongozi wa jadi wa Wamwela, Chief Nakyoto Ismail Hassan Malibiche, alisisitiza umuhimu wa kudumisha amani na utulivu katika kipindi chote cha uchaguzi, akiwataka Watanzania kuchagua viongozi kwa njia ya amani bila kushawishika kuingia kwenye vurugu au machafuko.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo, aliwataka wananchi kuwa waangalifu dhidi ya wanasiasa na wanaharakati wanaotumia uchaguzi kama fursa ya kuleta vurugu na kuvuruga amani ya nchi.
Ibada hiyo ya maombi imeonyesha mshikamano wa kijamii na kuthibitisha dhamira ya wananchi wa Nachingwea kushiriki uchaguzi kwa njia ya kidemokrasia, salama na yenye tija kwa taifa zima
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.