Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amewataka wawekezaji mbalimbali kujitokeza kuwekeza kwenye fursa lukuki zinazopatikana Mkoa wa Lindi
Makamu wa Rais ameyasema hayo jana katika hotuba yake iliyosomwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe wakati wa ufungauzi wa kongamano la fursa za uwekezaji na Biashara lilofanyika katika hoteli ya Sea view iliyopo Manispaa ya Lindi
“Mkoa huu una ardhi kubwa inayofaa kwa kilimo , maeneo yanayofaa kwa shughuli za utalii wa mambo ya kale, uwindaji wa wanyama, uvuvi mkubwa baharini na ufugaji” Aliongeza mama Samia
Amesema kongamano hilo litasaidia kuanzisha mahusiano mapya katika biashara na uwekezaji katika Mkoa huo ambapo wenye mitaji watapata fursa ya kupata taarifa za fursa zilizopo
Mapema akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi amesema mkoa unakaribisha wawekezaji kwa kuwa una fursa nyingi na uwekezaji ambazo nyingine hazijaguswa kabisa.
“Mkoa una ardhi ya kilimo ekari 5000 ambapo kati hizo ni ekari 2000 tu ndio zilizotumika, kuna amani ya kutosha, kuna bichi nzuri ambazo hazijachafuliwa, kuna mji wa Kilwa ambao ndio mji wa kwanza kutumia hela yake wenyewe” Alisema Mheshimiwa Zambi
Jukwaa la fursa za uwekezaji limeandaliwa nakampuni ya magazeti ya Serikali TSN kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwa lengo la kuibua na kutangaza fursa za uwekezaji zinazopatikana katika mkoa huo.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.