• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua za Watumishi |
    • Malalamiko/mrejesho |
Nachingwea District Council
Nachingwea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii Vijana na Ustawi wa Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Mkaguzi wa ndani
      • Uchaguzi
      • TEHAMA
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Ugani
  • Madiwanii
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Utawala Mipango na Fedha
      • Ujenzi uchumi na mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari

BARAZA LA MADIWANI WAJADILI CHANGAMOTO YA TEMBO, MGODI WA NDITI NA FEDHA ZA MFUKO WA ELIMU

Imetumwa : May 5th, 2023

Baraza la madiwani robo ya tatu mwaka wa fedha 2022 /2023 la wilaya ya Nachingwea limefanya mkutano wa baraza baada ya kutanguliwa na vikao vya kamati na uwasilishaji wa taarifa za kata.   Katika mkutano huo waheshimiwa madiwani wameweza kujadili maswala kadhaa yanayohusu maendeleo ya wilaya yakiwemo kuchelewa kwa pembejeo za kilimo katika msimu husika ambapo waheshimiwa wamemsisitiza Mkurugenzi kuchukua hatua za makusudi katika kuhakikisha mbolea inawafikia wananchi mapema kupitia idara ya kilimo . Kwa upande wa mkurugenzi. kupitia mkuu wa idara wa kilimo na umwagiliaji ametumia fursa hiyo kuwaomba waheshimiwa madiwani kwakuwa changamoto kubwa ni uhaba wa wazabuni wanaoweza kuchukua mzigo kwa wingi na kuja kuwauzia wananchi kwa bei nafuu, hivyo wavishawishi ama kuvishauri vyama vya msingi kutumia fursa hiyo ya kuchukua pembejeo na kuwauzia wakulima.

Mali na mjadala wa pembe jeo , waheshimiwa madiwani wamejikita hasa katika kutafuta suluhu ya changamoto kuu tatu, ambazo ni namna ya kuwadhibiti tembo na athari zake, Kuomba ufafanuzi wa matumizi ya fedha za mfuko wa elimu na udhibiti wa mapato ya mgodi wa nditi.

Waheshimiwa madiwani wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Lindi kushiriki kikao cha baraza maalum la Halmashauri ya Nachingwea kwa ajili ya ufafanuzi na kujadili matumizi ya fedha za mfuko wa elimu ambao unatokana na makato ya mazao ya biashasra hasa korosho.Waheshimiwa madiwani wamefikia uwamuzi huo kutokana na agizo la Mkuu wa Mkoa  la kuzitaka halmashauri za Mkoa wa Lindi kutumia  fedha za mfuko wa elimu kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwa ujumla wake na siyo kuzigawa kila kata kulingana na walichochangia.

Akichangia diwani wa kata Marambo Mhe. Selemani Katali amesema kubadilishwa kwa matumizi kwa fedha hizo kunaleta changamoto kubwa kwa wananchi kwani matarajio ya wananchi katika kila kata kuona fedha hizo zinashuka katani kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya ndani ya kata kulingana na kilichochangiwa . Hivyo agizo hilo linahitaji mjadala na ufafanuzi wa kina kuhusu kubadilishwa kwa matumizi .

Mwenyekiti wa halmashauri  Mhe. Adinani Mpyagila aliwaeleza waheshimiwa madiwani kuwa kupitia kikao cha kupitia taarifa za shughuli za maendeleo kwenye kata, makubaliano kuwa aombwe Mkuu wa Mkoa kushiriki baraza maalum kwa ajili ya ufafanuzi wa kubadilishwa kwa matumizi ya fedha hizo. Taarifa hiyo iliungwa mkona wa wajumbe na kuridhia kuombwa kwa mkuu wa mkoa katika baraza hilo.

Kwa upande wa changamoto ya tembo ambayo inaathiri baadhi ya wananchi wa wilaya ya Nachingwea , baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Nachingwea limeiomba serikali kuanza kuitumia helikopta kwa dharura kwa lengo la kuokoa jamii kutokana na uaribifu wa mazao na vifo kwa wananchi.

Akichangia mada ya tembo diwani wa kata ya Ngunichile Mhe.  Said Makayola amesema baraza linapaswa kuchukua hatua za haraka katika kutatua changamoto ya tembo kwani hali ni mbaya kwa wananchi.

Kutokana na michango ya waheshimiwa madiwani , Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Adinani Mpyagila akidhibitisha uwepo wa kadhia hiyo, ameiomba serikli kuona umuhimu wa kutumia helikopta kwa dharura kwa lengo la kunusuru jamii, kwani njia hiyo imekuwa msaada wa haraka kwa sasa wakati njia ya kudumu ya kutatua changamoto hiyo inaendelea kuwekwa sawa.

Matangazo

  • ORODHA YA WANAOITWA KWENYE MAFUNZO YA ANWANI ZA MAKAZI March 26, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA WATENDAJI WA KIJIJI III NAFASI 16 NA DERAVA DARAJA II NAFASI NNE May 25, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WALIOOMBA AJIRA ZA UTENDAJI WA KIJIJI NA UDEREVA HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA July 22, 2022
  • Tangazo la kazi za muda December 27, 2019
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WANAFUNZI WA NACHINGWEA HIGH NA RUGWA BOYS WAAGWA KWA HAFLA FUPI, WAJIANDAA KWA MITIHANI YA TAIFA

    April 26, 2025
  • SDA NA LIIKE WATOA MAFUNZO YA HUDUMA YA KWANZA KWA MANGALIBA NA WALOMBO KWA AJILI YA KUIMARISHA UTAMADUNI SALAMA

    April 28, 2025
  • DED NACHINGWEA : AAGIZA MIRADI KUKAMILIKA KWA WAKATI NA KWA KUZINGATIA VIWANGO

    April 09, 2025
  • RC LINDI : MIRADI YOTE ITAKAYOPITIWA NA MWENGE IZINGATIE MATUMIZI BORA YA FEDHA

    April 05, 2025
  • Angalia zote

Video

Wakulima wasisitizwa kulima mazao ya chakula
Video za mpya

Kurasa za Haraka

  • Opras Form
  • Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nachingwea Eng. Chionda Alli Mfaume akizungumza waluu wa idara
  • MRADI WA MAJI NAMIKANGO WAZINDULIWA
  • Mpango wa Bajeti
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2021
  • UANZISHWAJI WA BLOCK FARMING WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA
  • MRADI WA MAJI WA ZAIDI YA BILIONI 1 WAANZA KUTEKELEZWA NAIPANGA
  • Sheria za Fedha za Mitaa
  • Sheria za Halmashauri

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • TUZO ZA ELIMU WILAYA YA NACHINGWEA
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.