Kikao cha Robo ya Nne ya mwisho wa mwaka kilichoketi kwa ajili ya kujadili maswala mbalimbali yanayohusu Halmashauri ya Nachingwea.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. Adinani Mpyagila amewapongeza waheshimiwa madiwani na wataalamu kwa michango yao chanya ambayo inasaidia halmashauri kusonga mbele kwa hatua kubwa ya kimaendeleo.
Baraza limejipanga kusimamia mikakati, na mipango yake iliyowekwa katika sekta ya Elimu, Afya, Miundombinu ya Brabara, hali ya Chakula, madhara ya tembo na namna ya kuwaondoa, uthibiti wa utoroshaji wa mazao ya biashara nje ya wilaya ya Nachingwea, hali hii maambukizi ya TB na upimaji wake, Mji na hamasa ya Sensa ya watu na makazi itakayofanyika agosti 23, 2022.
Aidha , Mhe. Mwenyekiti amaewataka watumishi wa umma kuendelea kuwa waadilifu katika utumishi wao.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.