Zao la tunda la tikiti maji limegeuka kuwa lulu katika maonyesho ya nane nane kanda ya kusini baada kutengenezwa na kuwa asali kama zilikuwa asali nyingine.
Akizungumza kwenye maonyesho hayo mjasiriamali Zaituni Mahonda alisema kuwa baada ya kuugua muda mrefu vidonda vya tumbo ndio aliambia na mtaalamu wa afya kuwa asali ya tikiti inatibu haraka vidonda vya tumbo ndipo alipoanza kuitengeneza na kuitumia na kumpa matibabu yeye na familia yake.
Mahonda alisema kuwa asali hiyo inatibu vidonda vya tumbo na magonjwa mengine kutokana na ubora wa virutubisho vilivyomo kwenye tunda la tikiti maji.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.