• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua za Watumishi |
    • Malalamiko/mrejesho |
Nachingwea District Council
Nachingwea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii Vijana na Ustawi wa Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Mkaguzi wa ndani
      • Uchaguzi
      • TEHAMA
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Ugani
  • Madiwanii
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Utawala Mipango na Fedha
      • Ujenzi uchumi na mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari

MASHARTI YA KUPATA LESENI YA BIASHARA

 

 

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA

SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA WILAYA YA      NACHINGWEA

   

 

                                               

 

LESENI YA BIASHARA 

MASHARTI YA KUPATA LESENI YA BIASHARA

Mtu yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya biashara ili mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane (18) mwenye akili timamu ambaye hajawai kupatikana na kosa la jinai na awe na eneo la kufanyia biashara linalokubalika kisheria.

Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya biashara nchini kutoka idara ya uhamiaji.

UTARATIBU WA KUPATA LESENI YA BIASHARA

 

MWOMBAJI KAMA NI KAMPUNI ANATAKIWA KUWA NA NAKALA ZIFUATAZO:

Mwombaji anapaswa kujaza fomu ya maombi 9TFN2110 kikamilifu na kuambatanisha kivuli cha:

  • Hati ya Mlipa kodi (TIN) toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
  • Cheti cha Mlipa kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (Tax Clearance Certificate)
  • Usajiri wa jina la biashara toka Brela (Business Name)
  • Hati ya Usajili wa Kampuni (Certificate of Incorporation or Registration).
  • Memelanda ya kampuni (´´Memorandum and Article of Association´´).
  • Wasifu wa Kampuni (Company Profile)
  • Hati ya kiuwakili (Power of a Hatoney) kama wenye hisa wote wa kampuni wapo nje ya nchi.
  • Kwa biashara zinazodhibitiwa na mamlaka zingine za kisheria mfano; (TBS, EWURA, TAURA, CRB, TILLI, BODI YA MAGHALA, BODI YA NYAMA) n.k mwombaji anatakiwa kuwa na kibali au leseni ya kusajiliwa kwenye hiyo mamlaka husika kabla ya kuomba fomu ya maombi ya leseni ya biashara.

KAMA MWOMBAJI NI MTU BINAFSI

Mwombaji anapaswa kujaza fomu ya maombi 9TFN2110 kikamilifu na kuambatanisha kivuli cha:

  • Hati ya Mlipa kodi (TIN) toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
  • Cheti cha Mlipa kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (Tax Clearance Certificate)
  • Jina la biashara kama amesajili  toka  Brela (Business Name)
  • Kwa biashara zinazodhibitiwa na mamlaka zingine za kisheria mfano; (TBS, EWURA, TAURA, CRB, TILLI, BODI YA MAGHALA) n.k mwombaji anatakiwa kuwa na kibali au leseni ya kusajiliwa kwenye hiyo mamlaka husika kabla ya kuomba fomu ya maombi ya leseni ya biashara.

MASHARTI YA UTUMIAJI WA LESENI

  • Mwenye leseni hataweka masharti yeyote kwa mnunuzi.
  • Mwenye leseni atatoa stakabadhi/risiti  kwa mauzo yote.
  • Mwenye leseni atafuata sheria ya leseni ya biashara ya Mwaka 1972 na 1980.
  • Mwenye leseni hatauza huduma na bidhaa ambazo hazizingatii viwango vya ubora, vilivyowekwa na vyombo vinavyohusika kisheria.
  • Mwenye leseni anaweza kunyang`anywa wakati wo wote ikiwa itaonekana kwamba aliipata kwa  udanganyifu au amekiuka masharti ya leseni.
  • Mwenye leseni anatakiwa kutoa taarifa ya kimaandishi kwa Mkurugenzi mtendaji inapotokea biashara yake imepata changamoto iliyo nje ya uwezo wake na kumpelekea kushindwa kulipa ada ya leseni usika.

 

MAKOSA

  • Kuendesha biashara bila leseni ya biashara.
  • Mmiliki wa biashara au yeyote aliyemwachia Kumzuia afisa wa serikali mwenye mamlaka ya kukagua au aliyepewa kufanya kazi yake ya ukaguzi katika  biashara yake.
  • Kuendesha biashara eneo tofauti na lilooneshwa kwenye leseni.
  • Kutumia leseni moja kufanyia biashara zaidi ya moja au maeneo mawili au zaidi.
  • Kushindwa kuonesha leseni ya biashara inapotakiwa kufanya hivyo na afisa mwenye mamlaka au alioidhinishwa na serikali.
  • Kutokuweka leseni ya biashara mahali ambapo inaonekana kwa urahisi.
  • Kutoa maelezo ya uongo ili kujipatia leseni, kwa lengo la kukwepa kulipa ada ya leseni au tozo inayostahili.
  • Kumshambulia kwa kutoa lugha chafu afisa wa serikali mwenye mamlaka au aliyepewa kazi ya kukagua biashara yako.
  •  

 

  •  

  • ADHABU
  • Mtu yeyote anayetenda mojawapo ya makossa hayo hapo juu adhabu yake ni faini isiyopungua Tzs. 50,000.00 na isiyozidi Tzs. 100,000.00 au kifungo kisichozidi miaka miwili (2) au faini na kifungo vyoote kwa pamoja.
  • LESENI ZA VILEO (LIQUOR LICENSE)
  •                  THE INTOXICATING LIQUORS ACT (CAP 77 R.E.2002)
  •                                                                        
  • Sheria za vileo The Intoxicating Liquor Act (CAP 77 R.E.2002) imenyambulisha aina tisa za leseni za vileo zinazoweza kutolewa chini ya sheria hii.
  • RETAILERS ON (BAA)
  • Leseni hii humru husu mwenye biashara kuuza pombe na kunywa eneo la biashara.
  • MUDA 
  • MJINI
  • SIKU ZA KAZI (JUMATATU HADI IJUMAA)
  • Kuanzia saa 9:30 Alasiri hadi Saa 5:00 Usiku.
  • SIKU ZA MAPUMZIKO (JUMAMOSI, JUMAPILI SIKU ZA KITAIFA)
  • Kuanzia saa 8:00 Mchana hadi Saa 6:00 Usiku
  • VIJIJINI
  • SIKU ZA KAZI (JUMATATU HADI IJUMAA)
  • Kuanzia saa 9:00 Alasiri hadi Saa 2:00 Usiku.
  • SIKU ZA MAPUMZIKO (JUMAMOSI, JUMAPILI SIKU ZA KITAIFA)
  • Kuanzia saa 8:00 Mchana hadi Saa 5:00 Usiku
  •  
  • RETAILERS OFF(GROSARI)
  • Leseni hii haimruhusu mtu kunywea pombe eneo la biashara bali kwa watu wanaochukua kunywea majumbani. (Take away) kama Groceries.
  • WHOLESALE (UUZAJI WA JUMLA)
  • Leseni hii ni kuuza pombe kwa jumla.
  • SIKU ZA KAZI (JUMATATU HADI IJUMAA)
  • Kuanzia saa 2:00 Asbh hadi Saa 1:00 Usiku.
  • SIKU ZA MAPUMZIKO (JUMAMOSI, JUMAPILI SIKU ZA KITAIFA)
  • Kuanzia saa 3:00 Asbh hadi Saa 6:00 Mchana

          HOTEL

Leseni hii humruhusu mwenye leseni kuuza pombe kwa ajili ya     kunywea katika eneo la biashara kwa watu waliopanga hotelini kwa wakati wowote wa mchana na usiku.

RESTAURENT(MGAHAWA)

Leseni hii inamruhusu mwenye leseni kuuza pombe kwa mtu yeyote anayekula chakula katika mgahawa katika muda wa saa 6:00 Mchana hadi saa 8:00 Mchana na saa 12.00 Jioni hadi saa 6:00 Usiku.

MEMBERS CLUB(WANACHAMA)

Leseni hii huruhusu uuzaji wa pombe kwa kiasi chochote kwa mwanachama wa klabu na wageni wao tu.

COMBINED(MCHANGANYIKO)

Leseni ambazo zimeambatanishwa  mbili kwa pamoja:

  • 1.Combined Hotel and Retailers on.
  • 2.Combined Hotel and Restaurant.
  • 3.Combined Restaurant and Retailers on.
  •  
  • TEMPORARY (ISIYO YA KUDUMU/KIBALI)
  • Leseni hii humruhusu mwenye leseni kuuza pombe katika sehemu iliyotajwa kwenye leseni mahali penye burudani, starehe au mkusanyiko mwingine kwa kipindi kisichozidi siku tatu.
  • LOCAL LIQUOR
  •  
  • CLASS A: LOCAL LIQUOR
  • Leseni hii humruhusu mwenye leseni kutengeneza pombe za kienyeji katika sehemu iliyotajwa na kuuza kwa ajili ya kunywea sehemu ya biashara au nje ya sehemu ya biashara.
  • CLASS B: LOCAL LIQUOR
  • Leseni hii humruhusu kutengeneza pombe ya kienyeji sehemu iliyotajwa na kwenda kuuzia sehemu nyingine iliyo na leseni ya luuzia.
  •  
  • CLASS C: LOCAL LIQUOR
  • Leseni hii humruhusu kutengeneza pombe ya kienyeji katika sehemu iliyotajwa kwenye leseni na kuuza kwa mwenye class D Au Class E
  • CLASS D: LOCAL LIQUOR
  • Leseni hii humruhusu kuuza pombe za kienyeji katika sehemu iliyotajwa kwenye leseni kwa kunywea eneo la biashara.
  • CLASS E: LOCAL LIQUOR
  • Leseni hii humruhusu kuuza pombe za kienyeji kwa ajili ya kunywea sehemu nyingine mbali ya eneo la biashara.
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  • MASHARITI YA KUPATA LESENI YA VILEO
  • Mtu yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya Vileo ili mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane (18) mwenye akili timamu ambaye hajawai kupatikana na kosa la jinai na awe na eneo la kufanyia biashara linalokubalika kisheria. Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali kinachomruhusu  kufanya biashara nchini kutoka idara ya uamiaji.
  • UTARATIBU WA KUPATA LESENI YA VILEO
  • Mwombaji hujaza fomu za maombi zinazotolewa na Halmashauri.
  • Eneo au jengo linalokusudiwa kufanyiwa biashara hiyo kukaguliwa na afisa Mtendaji kata (WDC), afisa biashara,afisa afya, afisa Mipango Miji, Polisi na kutoa maoni yao kwenye fomu.
  • Maombi hayo hupelekwa katika mamlaka ya utoaji wa leseni za vileo ya Halmashauri kwa uamuzi.
  • Mwombaji ambaye maombi yake yamepitishwa hupewa leseni baadaya kulipa ada inayotakiwa na ni lazima amekamilisha masharti ya kupata leseni hapo juu.

            MASHARTI YA MTUMIAJI  

  • Kutouza kilevi kwa watoto chini ya umri wa miaka kumi na nane (18).
  • Kuzingatia muda ulioruhusiwa kisheria wa kuuza kilevi.
  • Muziki husiwakele watu wengine kwenye maeneo yao na uzingatie kibali alichoruhusiwa na afisa utamaduni wa Halmashauri.

MAKOSA

  • BAADHI YA MAKOSA CHINI YA SHERIA HII
  • Kutoweka leseni sehemu ya wazi , ambapo itaonekana kwa urahisi na wakaguzi.
  • Kuuza pombe kwa mtu mwenye umri chini ya miaka kumi na sinane (18) kukaa eneo la kuuza pombe.
  • Kuajiri mtu chini ya umri wa miaka kumi na nane (18) kuuza pombe.
  • Kuruhusu biashara nyingine isiyokubalika kisheria kufanya eneo la biashara.
  • Kuruhusu au kuleta fujo katika eneo la biashara.
  • Kuruhusu eneo la biashara kutumika kama danguro.
  • Kuuza pombe muda ambao ni kinyume cha sharia.
  • Kufanya biashara ya pombe kwa kutumia leseni ya vileo ambao haistahili.
  •  
  •  

ADHABU

Mfanyabiashara anayetenda mojawapo ya makossa haya akikamatwa, atafikishwa mahakamani na akikitiwa haiani atalipa faini au kifungo au adhabu zote kwa pamoja.

HOTEL LEVY

The Hotel Levy Act No.23/72

(The Hotel Levy Regulations – G.N.186/72)

 

HOTELI

Hoteli ni nyumba yoyote inayolala wageni kwa nia ya kuleta pato lakini,

(i)  Lazima iwe na wageni wasiopungua ishirini kwa ujazo wa nyumba hiyo.

(ii) Lazima iwe inatoa huduma za chakula kwa wageni wake.

(iii) Haitahusu nyumba za kulala wageni wa serikali (Government Rest House).

NYUMBA YA KULALA WAGENI (GUEST HOUSE)

  • Ni nyumba yoyote inayolala wageni kwa nia ya kuleta pato lakini bila kujali nambari ya wageni inafika wangapi lakini,
  •  
  • (i) Haitahusu nyumba za kulala wageni wa serikali (Government Rest House).
  • (ii) Haitoi huduma za chakula kwa wageni wake.
  •  

LESENI YA HOTEL NA NYUMBA ZA KULALA WAGENI

Mwombaji wa leseni ya Hotel na Nyumba za kulala Wageni atafafuata taratibu za kuomba leseni ya biashara kama zilivyoainishwa kwa mwombaji wa kampuni na mwombaji binafsi.

MASHARTI YA KUPATA LESENI YA BIASHARA

Mtu yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya biashara ili mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane (18) mwenye akili timamu ambaye hajawai kupaikana na kosa la jinai na awe na eneo la kufanyia biashara linalokubalika kisheria.

Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya biashara nchini kutoka idara ya uhamiaji.

  •  

MASHARTI YA UTUMIAJI WA LESENI

 

  • Mwenye leseni ya Hotel na Nyumba ya Kulalala Wageni au Mfanyakazi wake anatakiwa kuwa na daftari au kitabu ambacho kitatumiwa kujaza taarifa zote muhimu za wageni wanaolala.
  • Mwenye leseni ya Hotel na Nyumba ya Kulala Wageni anatakiwa kuwa na ulinzi imara katika biashara yake.
  • Mwenye leseni ya Hotel na Nyumba ya Kulala Wageni anatakiwa kuwa na mawasiliano na jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama na kutoa taarifa katika vyombo hivyo punde anavyokuwa na mgeni anaemtilia mashaka.
  • Mwenye leseni ya Hotel na Nyumba ya kulala wageni anatakiwa kufuata sheria ya Hotel Levy Act No.23/72.
  • Pamoja na mashariti hayo anatakiwa kufuata masharti ya leseni zingine kwa mujibu wa sheria ya leseni ya biashara ya Mwaka 1972 na marekebisho yake yam waka 1980. 
  • Mwenye leseni hataweka masharti yeyote kwa mnunuzi.
  • Mwenye leseni atatoa stakabadhi/risiti  kwa mauzo yote.
  • Mwenye leseni atafuata sheria ya leseni ya biashara ya Mwaka 1972 na 1980.
  • Mwenye leseni hatauza huduma na bidhaa ambazo hazizingatii viwango vya ubora, vilivyowekwa na vyombo vinavyohusika kisheria.
  • Mwenye leseni anaweza kunyang`anywa wakati wo wote ikiwa itaonekana kwamba aliipata kwa  udanganyifu au amekiuka masharti ya leseni.
  • Mwenye leseni anatakiwa kutoa taarifa ya kimaandishi kwa Mkurugenzi mtendaji inapotokea biashara yake imepata changamoto iliyo nje ya uwezo wake na kumpelekea kushindwa kulipa ada ya leseni usika.
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  • MAKOSA
  •  
  • Ni kosa kisheria mwenye leseni au mmiliki wa nyumba ya kulala wageni kutojaza au kusajiri taarifa za mteja au wageni kwa usahihi wanaolala kwenye nymba ya wageni.
  • Ni kosa kwa mmiliki wa nyumba ya kulalala Wageni kutunza waalifu kwenye biashara yake ya nyumba za kulala Wageni pamoja na wahamiaji haramu.
  • Ni kosa kwa mmiliki wa nyumba za kulala wageni kugeuza kuwa dangulo na kuhifadhi makahaba katika nyumba yake ya kulala wageni.
  • Ni kosa kufanya biashara bila kuwa na leseni ya biashara.
  • Ni kosa Kutokuweka leseni ya biashara mahali ambapo inaonekana kwa urahisi au katiaka eneo la biashara.
  • Ni kosa Mmiliki wa nyumba ya kulala Wageni au aliyemwachia Kumzuia afisa wa serikali mwenye mamlaka ya kukagua au aliyepewa kufanya kazi yake ya ukaguzi katika  biashara yake.
  • Ni kosa Kumshambulia kwa kutoa lugha chafu/matusi afisa wa serikali mwenye mamlaka au aliyepewa kazi ya kukagua biashara yako.
  •  
  • ADHABU
  •  
  • Mtu yeyote anayetenda mojawapo ya makossa hayo hapo juu adhabu yake ni faini isiyopungua Tzs. 50,000.00 na isiyozidi Tzs. 100,000.00 au kifungo kisichozidi miaka miwili (2) au faini na kifungo vyoote kwa pamoja.

 

Matangazo

  • ORODHA YA WANAOITWA KWENYE MAFUNZO YA ANWANI ZA MAKAZI March 26, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA WATENDAJI WA KIJIJI III NAFASI 16 NA DERAVA DARAJA II NAFASI NNE May 25, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WALIOOMBA AJIRA ZA UTENDAJI WA KIJIJI NA UDEREVA HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA July 22, 2022
  • Tangazo la kazi za muda December 27, 2019
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WANAFUNZI WA NACHINGWEA HIGH NA RUGWA BOYS WAAGWA KWA HAFLA FUPI, WAJIANDAA KWA MITIHANI YA TAIFA

    April 26, 2025
  • SDA NA LIIKE WATOA MAFUNZO YA HUDUMA YA KWANZA KWA MANGALIBA NA WALOMBO KWA AJILI YA KUIMARISHA UTAMADUNI SALAMA

    April 28, 2025
  • DED NACHINGWEA : AAGIZA MIRADI KUKAMILIKA KWA WAKATI NA KWA KUZINGATIA VIWANGO

    April 09, 2025
  • RC LINDI : MIRADI YOTE ITAKAYOPITIWA NA MWENGE IZINGATIE MATUMIZI BORA YA FEDHA

    April 05, 2025
  • Angalia zote

Video

Wakulima wasisitizwa kulima mazao ya chakula
Video za mpya

Kurasa za Haraka

  • Opras Form
  • Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nachingwea Eng. Chionda Alli Mfaume akizungumza waluu wa idara
  • MRADI WA MAJI NAMIKANGO WAZINDULIWA
  • Mpango wa Bajeti
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2021
  • UANZISHWAJI WA BLOCK FARMING WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA
  • MRADI WA MAJI WA ZAIDI YA BILIONI 1 WAANZA KUTEKELEZWA NAIPANGA
  • Sheria za Fedha za Mitaa
  • Sheria za Halmashauri

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • TUZO ZA ELIMU WILAYA YA NACHINGWEA
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.