FURUSA ZA BIASHARA HALMASHAURI YA WILAYA YANACHINGWEA
UTANGULIZI
Wilaya ya Nachingwea ipo umbali wa km 140 kutoka makao makuu ya mkoa wa Lindi , ipo kati ya nyuzi 10 - 11 Latitude kusini mwa ikweta , nyuzi 38 - 39 longitudo mashariki mwa griniwich.Nachingwea inapakana na Wilaya ya Ruangwa kwa upande wa kaskazini - mashariki ,Wilaya ya Masasi upande wa Kusini - mashariki ,Wilaya ya Tunduru upande wa kusini -magharibi na Wilaya ya Liwale upande wa Kaskazini - magharibi.Wilaya zingine zilizopo katika Mkoa wa Lindi ni Wilaya ya Kilwa, Manispaa ya Lindi na Wilaya ya Lindi Vijini.
WAKAZI
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.Wilaya ya Nachingwea ilikuwa na Jumla ya wakazi wapatao 178,464 ambapo 86,382 wavulana na 92,082 wanawake
UCHUMI
Pato la jumla la wakazi wa Nachingwea (GNP) kwa mwaka 2015/2016, lilikuwa Tshs 65,139,360,000/= (Bilioni sitini na tano milioni mia moja thelethini na tisa mia tatu sitini elfu tu.) Wastani wa pato la wakazi wa Nachingwea (Per Capital income) kwa mwaka 2015/2016 lilikuwa Sh 365,000/= kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Nachingwea ina ardhi yenye rutuba, hivyo kuwezesha uzalishaji wa mazao mengi ya chakula na biashara. Fursa hii itasaidia Wilaya yetu kutimiza dhana ya ‘KAZI IENDELEE’ na hatimae kufikia malengo ya uchumi wa kati. Katika kutekeleza majukumu ya kuinua uchumi, kupitia
|
|
Kufungua biashara Mjini na Vijijini:
Biashara za maduka ya rejareja.
Biashara za maduka ya nusu jumla.
Biashara za maduka ya jumla.
Biashara za vileo.
Biashara za nyumba za wageni.
Biashara za kumbi za mikutano.
Biashara za maduka ya pembejeo za kilimo.
Biashara za maduka ya dawa muhimu.
Biashara za maghala ya kuhifadhia mazao.
Biashara ya kufungua Kiwanda.
Biashara ya kufungua Shule binafsi.
Biashara ya kufungua Vyuo binafsi.
Biashara za vituo vya kuuza mafuta.
Biashara za kuuza nafaka.
Biashara za maduka ya vifaa vya ujenzi.
Biashara ya Vituo Vya afya na hospitali binafsi.
Biashara ya Super Market.
Biashara za vifaa vya michezo.
Bank.
Biashara ya Uwakala wa Mabenki.
Biashara ya fedha kupitia uwakala wa mitandao ya simu.
Kuuza mitungi ya gesi na majiko ya gesi.
Na biashara nyinginezo.
|
|
3.0 HALI YA UTOAJI WA LESENI ZA BIASHA NACHINGWEA
S/N
|
MWAKA |
IDADI YA LESENI |
PATO LINALOTOKANA NA ADA ZA LESENI ZA BIASHARA |
1.
|
2015/2016 (JULAI /JUNI)
|
732
|
32,783,400.00
|
2.
|
2016/2017 (JULAI / JUNI)
|
755
|
40,185,000.00
|
3.
|
2017/2018 (JULAI / JUNI)
|
696
|
33,520,500.00
|
4.
|
2018 /2019 (JULAI/JUNI)
|
791
|
40,474,000.00
|
5.
|
2019/2020 (JULAI/JUNI)
|
446
|
27,761,600.00
|
6.
|
2020/2021 (JULAI/JUNI)
|
350
|
29,566,000.00
|
7.
|
2021/2022(JULAI/SEPTEMBA……..)
|
181
|
16,864,000.00
|
CHATI KUONESHA HALI YA MAKUSANYO YATOKANAYO NA ADA ZA LESENI ZA BIASHARA KATIKA WILAYA YA NACHINGWEA
CHANGAMOTO
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
MASOKO
Nachingwea ina jumla ya masoko manne yanayomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea.Wanachi upata mahitaji yao mbalimbali kutoka katika masoko hayo. Mji wa Nachingwea Wakazi wake Wanaongezeke na hivyo kutakuwa na ongezeko la Masoko kadri idara ya Maliasili na ardhi inavyopima viwanja vya makazi ya Watu. Masoko yaliyopo kwa sasa ni:
1. SOKO KUU NACHINGWEA
2. SOKO LA VODA
3. SOKAO LA TUNDURU YA LEO
4. SOKO LA MATUNDA.
MABENKI
Nachingwea ina jumla ya benki tatu zinazotumiwa na wakazi wa Nachingwea.Kukua kwa teknolojia kumesaidia shughuli za kibenki kujitanua na kutoa furusa za wananchi kujiajiri kwa kuwa na Mawakala wa benki katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Nachingwea na kuwarahisishia wananchi kufanya malipo ya ankara mbalimbali, kutuma na kupokea fedha toka ndani na nje ya Nachingwea. Benki hizi ni:
1. NMB
2. CRDB
3. TCB
HUDUMA ZA FEDHA (MICROCREDIT)
Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea ina watoa huduma za kifedha (microcredit) wanaotambuliwa na serikali kwa leseni walizonazo toka Benki kuu ya Tanzania (BoT) na Brela wapatao kumi na moja ambao ofisi zao zipo Nachingwea Mjini katika mitaa tofautitofauti. Watoa huduma hawa utoa mikopo yao ya fedha kwa watumishi na watu mbalimbali na hivyo husaidia sekta ya biashara kwa wanufaika wa mikopo inayotolewa. Watoa huduma waliopo kwa sasa ni:
1.ABC BANK
2. MABOTO ENTERPRISES
3. SUMUNI CREDIT
4. CHOGO CREDIT
5. MAGERE CREDIT
6. WILIUM CREDIT
7.WICOM FINANCE LTD
8. TATA CREDIT
9. PLATNUM CREDIT
10. SILVER MICROFINANCE
11. FAIDIKA
MITANDAO YA MAWASILIANO
Halmashauri ya Nachingwea ina jumla ya mitandao ya mawasiliano sita na kufanya mawasiliano kupatikana kwa simu za kiganjani kwa wakazi wengi wanaoishi maeneo mbalimbali ya Nachingwea kuwasiliana kwa urahisi wakati wote. Aidha kupitia mitandao ya simu wanachi utumia fursa hiyo kujiajiri kwa kuwa Mawakala na kuwarahisishia wanachi kupata huduma ya kutuma na kupokea pesa kwa ndugu na marafiki kwa njia ya simu katika maeneo mbalimbali ya nachingwea nan je ya Nachingwea. Mitandao ya mawasiliano iliyopo kwa sasa ni:
1. TIGO
2. VODA
3. AIRTEL
4. HALOEL
5. TTCL
6. ZANTEL
4.0 HALI YA UWEKEZAJI
HALI YA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MADINI
Wilaya ya Nachingwea ni Wilaya iliyobarikiwa kuwa na madini ya aina nyingi. Kiwango cha uwekezaji kwa maana ya umiliki wa leseni za utafiti na uchimbaji/uchakataji pamoja na leseni za biashara ya madini ni cha chini. Miradi mingi ya utafiti na uchimbaji wa madini haiendelezwi ili kufikia hatua ya uchimbaji na hata wawekezaji wengi wenye leseni ndogo za uchimbaji hawazifanyii kazi (undeveloped).
Mada hii inalenga kuainisha aina za madini na maeneo yaliyopo katika Wilaya ya Nachingwea, fursa mbali mbali za uwekezaji zilizopo katika sekta ya madini katika Wilaya ya Nachingwea, pia taarifa hii itapambanua shughuli mbalimbali zinazofanyika katika sekta ya madini katika Wilaya hii. Na mwisho itabainisha changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta ya madini katika Wilaya ya Nachingwea na kutoa maoni ya namna ya kutatua changamoto hizo.
AINA ZA MADINI ZINAZOPATIKANA KATIKA WILAYA YA NACHINGWEA
Madini yaliyopo katika Wilaya ya Nachingwea ni madini ya metali, vito, viwandani na madini ya ujenzi. Jedwali namba 1 linaonesha maeneo mbalimbali madini hayo yanapopatikana na hali halisi ya kinachoendelea kwa sasa katika maeneo hayo.
Jedwali na. 1: Aina za Madini yaliyopo katika Wilaya ya Nachingwea
AINA YA MADINI
|
ENEO/KIJIJI
|
HALI YA UCHIMBAJI
|
Dhahabu (Gold)
|
Mto Mbwemkuru,
Ngapa, Ikungu, Maguja, marambo |
Uchimbaji unafanyika
|
Saphire
|
||
Ulanga, Cobalt, Nikeli, Magnesite
|
Nachingwea
|
Uchimbaji haufanyiki
|
Nikeli, Shaba, Cobalt
|
Lionja
|
Uchimbaji haufanyiki
|
Ulanga
|
Kitati
|
Uchimbaji haufanyiki
|
Kinywe (Graphite), Marble
|
Mkotokuyana
|
Uchimbaji haufanyiki
|
Kinywe (Graphite)
|
Chilunga
|
Uchimbaji haufanyiki
|
Ulanga
|
Mianganda
|
Uchimbaji haufanyiki
|
Ulanga
|
Mbuti
|
Uchimbaji haufanyiki
|
Kinywe (Graphite)
|
Nammanga
|
Uchimbaji haufanyiki
|
Nikeli, Shaba, Cobalt
|
Ntaka
|
Uchimbaji haufanyiki
|
Ulanga
|
Majiane
|
Uchimbaji haufanyiki
|
Kinywe (Graphite)
|
Chilunga
|
Uchimbaji haufanyiki
|
Mchanga, Kifusi, mawe
|
Nachingwea
|
Uchimbaji unafanyika
|
FURSA ZILIZOPO KATIKA SEKTA YA MADINI
Umiliki wa leseni za Kuchimba (SML, ML, PML)
Umiliki wa leseni za biashara ya Madini (Brokers na Dealers)
Umiliki wa mitambo ya kuchenjulia madini (cyanidation plant)
Umiliki wa mitambo ya uchimbaji kwa ajili ya kukodisha
Ufundi mitambo; mfano winchi, magari na mitambo ya aina nyingine
Chakula: Migahawa, hoteli na Mama Lishe
Ardhi/Nyumba: Ununuzi au ukodishaji wa maeneo kwa ajili ya uchimbaji, makazi au shughuli za kiufundi
Usafiri: Uwepo wa shughuli za usafirishaji
Kinachoendelea kwa sasa
AINA YA LESENI
|
IDADI YA LESENI
|
HALI YA SASA (STATUS)
|
MAELEZO
|
RL
|
1
|
MAANDALIZI YA KUJENGA MGODI
|
Leseni hii ni mali ya Serikali anatafutwa mzabuni wa kuwekeza katika eneo hili.
|
ML
|
03
|
UCHIMBAJI/ MAANDALIZI YA KUJENGA MIGODI
|
Kumekuwa na hali ya kusua sua katika uendelezaji wa miradi hii.
|
PL
|
21
|
UTAFITI
|
Kumekuwa na hali ya kusua sua katika uendelezaji wa miradi hii.
|
PML
|
199
|
UCHIMBAJI/ LIOLALA (DORMANT)
|
Ufutaji wa leseni zisizoendelezwa unaendelea kwa mujibu wa sheria.
|
Dealers
|
1
|
- |
- |
Brokers
|
4
|
- |
- |
MASOKO YA MADINI
|
VITUO VYA UNUNUZI (BUYING CENTRES)
|
MAELEZO
|
SOKO LA MADINI RUANGWA
|
NAMUNGO- DHAHABU/ VITO
|
|
|
KIEGEI-DHAHABU/ VITO
|
|
Na.
|
Changamoto
|
Hatua iliyochukuliwa
|
Mkakati
|
1.
|
Umbali wa eneo la kununulia milipuko (baruti, n.k.) ambao huongeza gharama za kusafirisha mara kwa mara hasa kwa wachimbaji wadogo.
|
Umefanyika uwekezaji katika eneo la karibu (Kilwa) na kampuni ya Nitro Explosives.
|
Kumwezesha mwekezaji huyu kuanza uzalishaji mapema iwezekanavyo
|
2.
|
Barabara kutoka maeneo ya uchimbaji sio nzuri na hazipitiki muda wote. Hali hii husababisha wachimbaji wengi kusimamisha shughuli za uzalishaji kipindi cha mvua.
|
Uandaaji wa mpango wa ujengaji yadi katika maeneo ya uchimbaji ambapo barabara kutoka machimboni hadi kwenye yadi na kutoka kwenye yadi hadi barabara kuu zitaboreshwa ziweze kupitika muda wote.
|
Kuwashirikisha wadau wote (Wachimbaji na wenye viwanda) katika kuchangia ili kupata fedha za kufanikisha mpango huu
|
3.
|
Ufinyu wa mitaji (kusababisha gharama za uzalishaji kuwa kubwa, hasa kwa PMLs (Prod.Cost/tonne)-kushindwa kutengeneza miundo mbinu, kufanya kazi miezi michache kwa mwaka kusimamisha uzalishaji wakati wa mvua), kukodi mitambo kwa zamu.
|
Utaratibu wa kutoa elimu juu ya fursa mbalimbali za kupata mikopo katika taasisi za fedha umekuwa ukifanyika kwa kushirikiana na taasisi za kifedha.
|
|
4.
|
Kutokuwa na tabia ya kuweka kumbukumbu za uzalishaji wa na gharama zake hivyo kushindwa kupata mikopo lakini hata wanapopata mikopo hushindwa kulipa kutokana na kushindwa kutambua faida ni kiasi gani hali ambayo husababisha kufilisika.
|
Wachimbaji wameendelea kupatiwa elimu ya namna ya kuendesha biashara zao.
|
|
5.
|
Ukosefu wa viwanda vya kupandisha thamani (Refining) kusababisha madini mengine kutochimbwa kabisa Mn, Cu, Co etc.
|
Uhamasishaji uliofanywa na Serikali umeanza kuonesha mafanikio kwa viwanda vidogo vya kusafisha shaba kujengwa nchini na hivyo uchimbaji wa shaba ghafi kuwa na soko la uhakika.
Hivi karibuni Serikali imefanya marekebisho katika muongozo uliokuwa unatumika ambao una taratibu za uongezaji thamani “Mining (Value Addition) Regulations, 2020 ambapo imelegeza masharti ili kuwawezesha wachimbaji wadogo wasikwame. |
Kuendelea kuhamasisha iliuwekezaji zaidi kwa madini mengine ufanyike
|
MAZAO YA BIASHARA
HALI YA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA KILIMO ZAO LA KOROSHO
Hali ya uzalishaji wa zao la korosho
S/Na
|
MWAKA
|
TANI
|
1
|
2017/2018
|
21
|
2
|
2018/2019
|
16
|
3
|
2019/2020
|
16
|
4
|
2020/2021
|
22
|
5
|
2021/2022
|
23
|
MIKAKATI YA KUENDELEZA UWEKEZAJI ZAO LA KOROSHO
Wilaya inafanya juhudi nyingi kuhakikisha uwekezaji mkubwa unafanyika. Juhidi hizo ni pamoja na kuanzisha mradi wa mbegu bora za zao la korosho kijiji cha Likwela kata ya Mkoka (mradi huu ushaanza msimu uliopita wa kilimo 2020/2021). Juhudi nyingine ni pamoja na kuendeleza viwanda na kuongeza ufanisi katika viwanda vya korosho.
4.2 UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA KILIMO ZAO LA UFUTA
Hali ya uzalishaji wa zao la ufuta
S/Na
|
MWAKA
|
TANI
|
1
|
2017/2018
|
2,383
|
2
|
2018/2019
|
4,070
|
3
|
2019/2020
|
8,500
|
4
|
2020/2021
|
10,300
|
5
|
2021/2022
|
7,493
|
MIKAKATI YA KUENDELEZA UWEKEZAJI ZAO LA UFUTA
Wilaya inafanya juhudi nyingi kuhakikisha uwekezaji mkubwa unafanyika. Juhidi hizo ni pamoja na kuanzisha mradi wa mbegu bora za zao la ufuta kijiji cha Likwela kata ya Mkoka (mradi huu utaanza msimu ujao wa kilimo). Juhudi nyingine ni pamoja na kuendeleza viwanda na kuongeza ufanisi katika viwanda vya korosho.
4.2 Uwekezaji katika sekta ujasiliamali vikundi vya ujasiriamali
Jumla ya vikundi 300 vya ujasiriamali vimesajiliwa. Vikundi hivi vinajishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi hasa Mama lishe, Bodaboda, VICOBA, kushona mavazi, ufugaji, kilimo, ufundi seremala, kuchomea chuma, usindikaji, kubangua korosho, uhunzi na uchongaji.
JEDWALI LA VIKUNDI VYA UJASILIA MALI
S/NA
|
IDADI YA VIKUNDI
|
SHUGHULI
|
1
|
15
|
Kilimo cha mbogamboga
|
2
|
40
|
Ufugaji
|
3
|
10
|
Korosho
|
4
|
2
|
Ufuta
|
5
|
19
|
Labourbase
|
6.
|
1
|
Vinyago
|
8.
|
1
|
Uhunzi
|
9.
|
212
|
Vikoba,Bodaboda,Mama Lishe,Kushona n.k
|
Jumla
|
300
|
|
4.3 Uwekezaji katika sekta ya viwanda
Jumla ya viwanda vidogo vidogo 134 vimesajiliwa hapa Wilayani.Shuguli kubwa ya viwanda hivi ni kutengeneza samani, ushonaji, usindikaji, Ubanguaji korosho na kusaga nafa.
JEDWALI KUONESHA VIWANDA
S/NA
|
KIWANDA
|
SHUGHULI
|
ENEO
|
1
|
1
|
Ubanguaji wa korosho
|
Nangowe
|
2
|
5
|
Kutengeneza samani
|
Eneo la viwanda, Mtua,T/Leo, Ugogoni
|
3
|
1
|
Kuhuisha vyupa vya maji safi vilivyotumika
|
Eneo la viwanda
|
4
|
127
|
Mashine za kusaga nafaka na cherehani
|
Mjini na Vijijini
|
Jumla
|
134
|
|
3.4 Uwekezaji katika sekta kilimo cha mbogamboga
Licha ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara, Wilaya pia ina maeneo makubwa na mazuri yanayofaa kwa kilimo cha mazao ya mbogamboga. Maeneo haya yana mabwawa ya umwagiliaji ila kuna changamoto ya uchakavu wa miundombinu
Jedwali 1: Maeneo ya kilimo cha mbogamboga
Na |
Eneo
|
Ukubwa wa eneo |
1. |
Matekwe
|
120 |
2. |
Mitumbati
|
50 |
3. |
Ntila
|
30 |
4. |
Bonde la Ruponda
|
20 |
|
Jumla
|
220 |
4.4 Uwekezaji katika sekta ya mifugo
Wilaya ina maeneo mengi na makubwa ya uwekezaji katika mifugo kama inavyoonekana kwenye Jedwali Na. 1.
Jedwali 2: Vijiji vilivyopimwa nakutengwa eneo la malisho
Na |
Kijiji
|
Idadi ya Hekta |
1 |
Likwela
|
2,352.17 |
2 |
Nakalonji
|
2,660.00 |
3 |
Chimbendenga
|
7,918.04 |
4 |
Kilimarondo
|
4,360.05 |
5 |
Namapwia
|
1,345.93 |
6 |
Mtua
|
1,836.81 |
7 |
Matekwe
|
14,318.89 |
8 |
Kiegei
|
2,337.32 |
9 |
Mbondo
|
2,144.87 |
10 |
Maziwa
|
2,096.32 |
11 |
Ngunichile
|
158.00 |
12 |
Nahimba
|
412.00 |
13 |
Namatunu
|
1,004.00 |
14 |
Majonanga
|
375.74 |
15 |
Makitikiti
|
370.00 |
16 |
Ndomondo
|
430.00 |
|
Jumla
|
44,120.14 |
Uwekezaji katika sekta ya Elimu
Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea ina utaratibu wa kuwa na mradi mkubwa wa kujenga shule kubwa ya sekondari itakayoanzia kidato cha kwanza hadi cha sita, utaratibu wa kupata eneo la ujenzi wa shule hiyo unaendelea mkuu wa idara ya ardhi na maliasili anaendelea na utaratibu huo.
5.5 Maeneo ya uwekezaji yaliyotengwa
Mbali na maeneo ya ufugaji, Wilaya ina maeneo mengi ya uwekezaji kama inavyoonekana kwenye Jedwali Na.2.
Jedwali 3: Maeneo ya uwekezaji
|
AINA YA UWEKEZAJI
|
MAHALI ENEO LILIPO
|
UKUBWA WA ENEO
|
1 |
ENEO LA VIWANDA
Viwanda viko kwenye ramani ya mipango miji taratibu za upimaji zinaendelea |
Bondeni Area
|
81,000m2
|
2 |
HOUSING ESTATE
Maeneo yamepimwa lakini hayajalipiwa fidia |
Bondeni Road
|
18,158m2 na 43,835m2 zipo kwe mpango wa upimwaji
|
3 |
MARKET
Eneo limeshapimwa tayari bado fidia |
Bondeni Road
|
22,704m2
|
4 |
SCHOOLS
Maeneo yapo yamepimwa tayari na pia yako mengine ambayo hayajapimwa |
Bondeni Road
|
83,481m2
|
5 |
MAENEO YA MADINI
Maeneo yametengwa maeneo yenye madini aina ya Dhahabu, Nickel, Chuma, Dhahaabu na Shaba. |
Kijiji cha Marambo
|
1,639.46m2
|
6 |
MISITU
Wilaya ina misitu yenye miti aina mbalimbali. Raslimali za misitu zinasimamiwa kwa mbinu shirikishi ya uhifadhi wa mazao ya misitu ambapo mpaka sasa kupitia programu ya PFM jumla ya misitu 9 imetambuliwa na kukabidhiwa kwa jamii za vijiji 11. |
Ndani ya Vijiji 11 kwa misitu 9
|
4,709,000 ha
|
7 |
UFUGAJI WA NYUKI
Kutokana na kuwepo na misitu ya asili ambayo inasaidia kuwepo kwa nyuki, Wilaya ina fursa ya kufuga nyuki kwa ajili ya kupata mazao yake ambayo ni muhimu kwa lishe. |
|
|
8 |
MAENEO YA UJENZI WA MAJUMBA
Yapo maeneo ambazo yamepimwa lakini hayajalipiwa fidia na maeneo menging yapo kwemye mpango wa upimaji |
Bondeni Road
|
18,158m2 na 43,835m2 zipo kwenye mpango wa upimaji
|
9 |
UTALII
Wilaya ina fursa kubwa ya uwekezaji hasa wa wanyamapori. Fursa hii pamoja na umuhimu wake haijaendelezwa ipasavyo na ikiendelezwa ni sehemu nzuri ya kihistoria ya ukombozi wa bara la Afrika hususani kwa nchi ya Msumbiji. |
Milima ya Ilulu, njia kuu ya wanyamapori toka Msanjesi hadi hifadhi ya wanyamapori ya Selous pamoja na kambi ya Farm 17 (Frelimo Freedom Fighters Camp).
Njia kuu ya wanyamapori ya Selous-Msanjesi ambayo ni kiunganisho na Lukwaka, Lumesule hadi hifadhi ya Nisassa iliyopo nchini Msumbiji |
|
10 |
MAENEO YA UJENZI WA SHULE
Yapo maeneo yaliyopimwa na yasiyopimwa |
Bondeni Road
|
83,481m2
|
|
ENEO AMBALO LIPO KWENYE UTAFITI
Yapo maeneo ambayo yapo kwenye utafiti madini ambayo yanapatikana ni Nickel, Iron, Gold na Copper. |
|
1607.94m2
|
Nia ya Wilaya ni kuona kila mwananchi anapata fursa ya uwekezaji katika moja ya maeneo yaliyoainishwa. Ni matumaini kuwa, fursa ya nchi yetu kuingia katika uchumi wa kati tutaitendea haki wana Nachingwea. Mshikamano wetu utaleta chachu kubwa katika kuinua uchumi wa Wilaya yetu na nchi kwa ujumla.
Shukrani kwa wakuu wa idara na vitengo, Taasisi za serikali kwa ushirikiano mlioutoa wakati mawasiliano ya kupata takwimu zilizotumika kuandaa tarifa hii.
IMEANDALIWA NA AFISA BIASHARA NACHINGWEA
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.