Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe;Godfrey Zambi amewahakikishia watumishi wa Mkoa wa Lindi kuwa Serikali inatambua mchango wao katika kutoa huduma kwa wananchi wa Mkoa huo na kufafanua kuwa itakuwa inaboresha maslahi yao kulingana na kuboreka kwa uchumi wa nchi.
Ameyasema hayo katika maadhimisho ya sherehe za siku ya wafanyakazi kimkoa iliyofanyika viwanja vya shule ya Msingi Likangala vilivyopo Wilayani Ruangwa.
Ameongeza kuwa Serikali kwa vipindi tofauti imekuwa ikibobresha maslahi ya watumishi ikiwemo kuongeza mishahara,kulipa madeni na pia kupunguza kodi kwenye mishahara kutoka asilimia kumi na saba (17) hadi tisa (9).
Aidha amewataka pamoja na watumishi kudai kuboreshwa kwa stahiki zao wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii kwenye maeneo yao na manung’uniko na masikitiko yao yasiwaathiri wale wanaowahudumia.
“Manung’uniko na masikitiko yenu yasiwaathiri wanafunzi kwani wote tusingefika hapa kama sio elimu”Aliongeza Mheshiwa Zambi.
Mapema akisoma risala ya wafanyakazi kwa Mkuu wa Mkoa, Mratibu wa Tucta Mkoa wa Lindi Fatma Chininga ameiomba serikali kuboresha maslahi ya watumishi ikiwemo mishahara,kupungunguza kodi kwenye mishahara,kujenga nyumba za watumishi na kulipa madeni kwa watumishi.
Kauli mbiu ya Mei Mosi mwaka huu ni ‘Uchumi wa viwanda uzingatie Haki,Maslahi na Heshima ya wafanyakazi’
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.