Leo, tarehe 3 Aprili, Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mheshimiwa Amandus Chinguile,akiambatana na kamati ya mfuko wajimbo ametembelea na kuweka jiwe la msingi kwenye Mradi wa Shule ya Msingi Mtuti iliyopo Kijiji cha Marambo A, Kata ya Marambo pamoja na Mradi wa Shule ya Msingi Mwanayamala Kijiji cha Mwananyamala Kata ya Ruponda kila moja ikiwa na thamani ya Milioni 334.6. Vilevile, alikagua ujenzi wa jengo la OPD katika Kituo cha Afya cha Majaliwa, kilichopo Kata ya Chiola, chenye thamani ya Milioni 193.4, ambapo hadi sasa Milioni 50.1 zimetumika.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mheshimiwa Chinguile ametoa shukrani kwa Rais kwa kutoa fedha za nyingi Wilaya ya Nachingwea amesisitiza miradi mingi imeletwa kwa miaka minne haijawahi kutokea.Amesema wananchi ilikua kilio chao Shule katika maeneo hayo sasa inaenda kuwa historia. Wananchi wa Marambo wanajivunia kuona shule hiyo ya kisasa ikikamilika, huku Mheshimiwa Mbunge akielezea kuridhishwa na kiwango cha ujenzi na kumpongeza Rais kwa utekelezaji wa miradi bora.
Wananchi wa Kata ya Ruponda pia walimshukuru Mheshimiwa Chinguile kwa kumheshimu kwa kuweka jiwe la msingi katika shule inayojengwa katika kata hiyo.Kata ambayo ndio anakoishi Mbunge huyo. Wameahidi kumpa kura za kutosha katika uchaguzi ujao kama shukrani kwa juhudi kubwa alizozifanya kwa maendeleo ya wilaya ya Nachingwea.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.