Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe. Hashim A. Komba ameagiza kupunguzwa kwa bei ya fomu za matibabu kwa wanafunzi ambao wanajiunga Kidato Cha Kwanza kutoka shilingi 18000 hadi elfu 4000 .
Mhe. Komba , ametoa agizo hilo leo Januari 12, 2023 alipofanya ziara kata ya Kipara Mtua yenye moja ya lengo la kubaini changamoto ya uripoti wa wanafunzi wa Kidato Cha Kwanza . Kufuatia kusuasua kwa uripoti wa wanafunzi ndani ya Wilaya ya Nachingwea ikiwemo kata ya Kipara Mtua Mhe. Komba akaagiza kupunguzwa kwa kiasi hicho Cha malipo ya fomu ya matibabu ikiwa ni sehemu ya kuwapunguzia mzigo wazazi na walezi wa Kuwapeleka watoto Shule .
Aidha, Mhe. Komba, ameagiza wanafunzi wapatiwe vipimo katika Zahanati au vituo vya Afya ambavyo vipo karibu navyo hakuna ulazima wa kutembea umbali mrefu kwenda katika Hospitali ya Wilaya kupata huduma hizo .
Katika hatua nyingine Mhe. Komba, amewataka wazazi hasa wanaume ambao wametelekeza familia zao na kushindwa kuwahudumia watoto ambao wamefaulu kujiunga Kidato Cha Kwanza waanze kuwahudumia kabla ya taratibu zingine za ufuatiliaji haziajaanza kuchukuliwa .
#Tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.