MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mhe Mohamed Moyo amewataka madiwani wa halmashauri kuhamasisha wananchi katika maeneo yao kuzingatia matumizi ya nishati safi ya gesi, ameyasema hayo Agost 1, 2024 alipokua kwenye mkutano wa baraza la madiwani la robo ya 4 ya mwaka wa fedha 2023/2024.
Mheshimiwa Moyo amesema mheshinmmiwa Rais Dokta Samia Suluhj Hassan amewataka wananchi kuacha kutumia kunk kwani zinachangia uharibifu wa mazingira na kuhatarisha maisha, badala yake amewataka wananchi kutumia nishati safi ya gesi katika kupimia.
Aidha,Mhe Moyo amewataka madiwani wahamasishe wananchi katika kata zao kujiandikisha na kushiriki katka uchaguzi wa serikali za mitaa , pia amewataka madiwani wahamasishe wananchi wa wilaya hiyo kuhusu uchukuaji wa mikopo ya 10% kwani serikali imeruhusu tena mikopo hiyo iendelee kutolewa kwa utaribu maalumu na kuwakumbusha kurejesha kwa wakati fedha hizo sambamba na hayo Mh huyo amewataka madiwani suala la lishe bora liwe ajenda katika vikao vyao vya maendeleo moo ili kutokomeza udumavu wa afya za wananchi.
@samia_suluhu_hassan
@ofisi_ya_makamu_wa_rais
@ortamisemi @msemajimkuuwaserikali
@maelezonews
@lindi_rs_
@wizara_ya_kilimo
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.