Wazee wa Nachingwea wameaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba mwaka huu Hayo yamebainishwa leo, Oktoba 3, 2024
Afisa Uchaguzi (W) wa Nachingwea ndugu Robert Mmari pia ameeleza kuwa sifa za mgombea na mpiga kura zimeshaainishwa Mpiga kura lazima awe na akili timamu, awe na umri wa miaka 18 au zaidi, na awe mkazi wa kitongoji husika Wananchi wote wanatakiwa kupiga kura kwenye vitongoji walivyojiandikisha, huku zoezi la kuchukua fomu za kugombea likipangwa kuanza Novemba 1
Aidha, ndugu Joshua Mnyang'ali, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Nachingwea, ametoa rai kwa mwananchi wote kujiandikisha kupiga kura kati ya Novemba 11 hadi 20, alisisitiza kuwa Halmashauri imejipanga vyema kuhakikisha wananchi wanapata elimu kuhusu uchaguzi na umuhimu wa kushiriki katika zoezi hilo
Kwa upande wake, Chief Nakotyo alibainisha kuwa kutakuwa na tukio maalum lenye ujumbe kuhusu maadili na hamasa ya uchaguzi litakalofanyika tarehe 7 na 8 Novemba hivyo amewataka wazee kuendelea kuhamasisha wananchi ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa mafanikio Vilevile, Joyce Chipanda, mkazi wa Kilimani Road, amewaasa wananchi kutopotosha wenzao na badala yake kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kulinda usalama na amani ya nchi
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.