Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea, Dkt. Shukurani Nsikini, ametambulisha kifaa kipya maalumu kwa ajili ya kukinga majengo ya hospitali dhidi ya athari za radi, hususan katika eneo la control room ambalo ni muhimu zaidi kwa kuwa ndilo linalosambaza umeme katika majengo yote ya hospitali.
Amesema kifaa hicho kinachojulikana kama lightning conductor kimefungwa mahsusi kuzuia madhara ya radi na imegharimu kiasi shilingi 600,000/ ikiwa ni sehemu ya juhudi za hospitali kuboresha usalama wa miundombinu yake ya umeme.
Dkt. Nsikini ameeleza kuwa katika kipindi cha mvua zilizopita, radi ilisababisha uharibifu wa mashine ya X-ray, hali ambayo ilisababisha wagonjwa kushindwa kupata huduma hiyo muhimu kwa muda kutokana na uharibifu uliotokea.
Kwa upande wake, fundi aliyefunga kifaa hicho, Abdul Mboneke, amesema kuwa kifaa hicho kitapunguza kwa kiasi kikubwa athari za radi, na kushauri hatua kama hiyo ichukuliwe pia katika majengo mengine ya hospitali ili kuongeza usalama na ufanisi wa huduma za afya.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.