Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea imeeleza fursa zinazopatikana kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali katika sekta ya madini ambapo kutaongeza chachu na muamko kwa wadau na wananchi kuwekeza katika sekta hiyo ambayo kuna fursa ya moja kwa moja inayowawezesha wawekezaji kupata leseni za kuchimba madini, kuchafanya biashara ya madini, fursa ya uchakataji na viwanda, fursa ya ushirika na biashara ndogondogo pamoja na fursa ya kuongeza thamani na utalii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri a Nachingwea Mhandisi Chionda M. Kwawa amewasihi Wadau na Mashirika mbalimbali kuangalia fursa na kuwekeza Wikayaninhumo, pia amesema "Nachingwea ya Madini itakua tofauti na kuwataka Watumishi pamoja na Wananchi kuitumia fursa hiyo vizuri, uchumi wa Nachingwea utakua na pato la Halmashauri litaongezeka".

Akizungumza na mwandishi wetu, Ndugu Azizi Katuli Kaimu Mkuu idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji amesema kuwa fursa hizo zina manufaa makubwa sana kwani huwezesha kutoa ajira za moja kwa moja kwa wananchi kama vile uchimbaji, usafirishaji na ulinzi, kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata leseni, kuongeza mapato ya serikali (kodi na michango).
Ndugu Katuli alisema, "Shughuli za kiuchumi na Kijamii zitakua na kubadilika hatutakuwa kama hivi tulivyo kwani fursa hii ya uwekezaji itafanya kuwe na ongezeko la watu na itapelekea wananchi kukuza biashara zao na kuleta mabadiliko chanya ya ujenzi wa miundombinu na huduma za kijamii".
Aidha, Ndugu Katuli ameeleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea imeweka mikakati ya kuongeza uhamasishaji kwa wananchi na ujenzi wa ujuzi katika sekta ya madini kupitia platifomu mbalimbali, kutoa mikopo ya asilimia kumi kwa vikundi kwa kutumia mapato ya ndani, kushirikiana na wadau kufanya maonyesho ya madini ili kuhakikisha wananchi wanapata manufaa yatokanayo na uwekezaji huo na kuleta maendeleo chanya katika jamii.
Ndugu Jonathan Kanji ambae ni mkazi na mjasiriamali wa Wilaya ya Nachingwea ametoa rai kwa wananchi na wafanyabiashara waweze kuchangamkia fursa hizo ili kuongeza maendeleo ya uchumi kwa maeneo wanaoishi huku akiwataka kuondokana na dhana potofu ya kwamba uwekezaji kwenye sekta ya madini hufanywa na watu kutoka nje ya nchi au wenye vipato vikubwa.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.