Septemba 9, 2025, Baraza la Wazee wilayani Nachingwea likiongozwa na Mwenyekiti wake Bi. Honoratha Chitanda limekutana na Msimamizi wa Uchaguzi kujadili maandalizi ya Uchaguzi Mkuu 2025. Kikao hicho muhimu kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea na kimebeba ujumbe mzito kuhusu amani, ushiriki na mshikamano wa kijamii.

Katika kikao hicho, wazee wamesisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa uchaguzi huru na wa haki. Wametaka hatua madhubuti zichukuliwe kuhakikisha kuwa kila hatua ya mchakato wa uchaguzi inazingatia utulivu na heshima kwa sheria.

Bi. Chitanda ametoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kushiriki katika uongozi, Vilevile, amewaomba wanaume kuwapa nafasi ya kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi, kwa sababu sauti ya kila mwananchi ni muhimu katika ujenzi wa taifa.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Uchaguzi bwana Joshua Mnyang'ali amewataka wazee kushiriki kwenye tamasha la One Stop Center litakalofanyika Okoba 1 hadi 3, 2025 ili walitumie kama fursa ya kuelimisha vijana kuhusu haki zao za kidemokrasia katika uchaguzi, amani, elimu, na ushirikiano wa vizazi vyote ni silaha madhubuti kuelekea uchaguzi wenye mafanikio.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.