Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo amewataka wazazi kuwekeza nguvu katika usawa wa kulea watoto wa kike na kiume, hayo ameyasema leo June 4, 2025 alipokua katika sherehe za ugawaji wa tuzo za elimu katika viwanja vya shule ya Msingi Majengo.
Mheshiwa Moyo amesisitiza ya kua, kulingana na mabadiliko makubwa ya kimaadili yaliyopo katika maisha ni wakati sasa kwa wazazi kuhakikisha watoto wote wa kike na kiume wanapewa malezi sawa ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, Wazazi wengi wamekua wakiweka nguvu kubwa kwa watoto wa kike pekee, jambo hilo limekua likiwaathiri sana watoto wa kiume.
Kwa upande mwingine amewasisitiza wazazi kufanya sana mazoezi ili kujiepusha na magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari, shinikizo la damu na mengine, kwani magonjwa haya yanapelekea watoto wengi kupoteza wazazi wote au mmoja na kuwaacha katika mazingira magumu.
Aidha, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ametoa pongezi kwa walimu, wazazi na wadau wote waliojitokeza katika kuupokea Mwenge wa Uhuru siku ya tarehe 29/05/2025 ulipofika katika Wilaya ya Nachingwea.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.