Watumishi watakiwa kuwa waadilifu, waaminifu na wabuinifu
Watumishi wa Mkoa wa Lindi wametakiwa kuwa waadilifu, waaminifu na wabunifu katika kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi wa mkoa huo
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Rehema Madenge jana wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Nachingwea katika ziara yake ya kujitambulisha na kukumbushana mambo mbalimbali ya kiutumishi.
“Watumishi wanatakiwa kufuata maadili na kanuni za utumishi wa umma ambazo zinatuka kuwahi na kukaa kazini muda wote, kutumia lugha nzuri kwa wateja, kuwa nadhifu na kuvaa mavazi ambayo yapo kwa mujibu wa waraka wa mavazi kwa watumishi wa umma” Alisema Madenge
Pia aliwataka wataalam wa Halmashauri kuweka dira itakayoleta mabadiliko chanya ili kuweza kupiga hatua katika maendeleo ya wilaya ya Nachingwea na mkoa kwa ujumla kwa kuanzisha miradi ya kimkakati itakayosaidia Halmashauri kuongeza wigo wa mapato.
Katika ziara yake Katibu Tawala katika ziara yake ameambatana na wakuu wa idara na vitengo mbalimbali ngazi ya mkoa kwa lengo la kujitambulisha na kuweka dira ya namna ya kutekeleza mambo mbalimbali katika kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Lindi
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.