Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary amewataka watumishi wa Mkoa wa Lindi kutumia fursa ya ushiriki wa Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma Kitaifa 2025 kujifunza mambo muhimu kutoka taasisi na Ofisi zingine zingine ambazo zimeshiriki Maadhimisho hayo.
Katibu Tawala ametoa wito huo leo Juni 22, 2025 alipotembelea viwanja vya maadhimisho hayo Chinangali Jijini Dodoma yaliyoanza Juni 16 na kutarajiwa kuhitimishwa Juni 23, 2025.
" ushiriki wetu katika Maadhimisho haya wamuhimu sana yanatupa fursa ya kujifunza kutoka kwa wengine hivyo tunapaswa kuzingatia na kuona wengine wanafanya nini ili kuwa bora katika utendaji wa kazi " Katibu Tawala Bi. Zuwena Omary .
Sambamba na hilo, amewapongeza watumishi wa mkoa wa Lindi kwa ubunifu na ushiriki wa Maadhimisho muhimu katika kuboresha utendaji wa kazi.
Awali, Katibu Tawala Msaidizi Utawala Ndugu Nathalis Linuma akitoa taarifa fupi ya namna mkoa wa Lindi ulivyoshiriki maadhimisho hayo , amesema Halmashauri zote za Mkoa wa Lindi zimeshiriki katika wiki ya utumishi wa umma na kila halmashauri imeweza kuonesha kitu cha tofauti katika kuboresha utoaji wa huduma kama vile One-Stop Centre kutoka Halmashauri ya Nachingwea, Utunzaji wa misitu kidigitali na mchakato wa uvunaji hewa Ukawaa kutoka Halmashauri ya Mtama, kadi_Alama kutoka Hospitali ya Mkoa ambayo inawezesha kuona na kuhamasisha utendaji wa kazi na fursa za uwekezaji zilizopo katika Halmashauri zote.
Aidha, Katibu Tawala Bi. Zuwena Omary, alimepata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ikiwemo TPDC ambapo ameweza kuona kupitia video namna mradi wa gesi LNG wa Lindi unavyotarajiwa kutekekezwa , mabanda mengine aliyotembele ni EWURA, LATRA, TFS ambako ameona na kupata tiba asili ya kudungwa na Nyuki na Mbeya RS.
Kwa upande wa Watumishi wa Mkoa wa Lindi wametumia fursa hiyo kumshukuru Katibu Tawala Mkoa kwa namna ambavyo ameandaa mazingira rafiki ya wao kushiriki wa maadhimisho hayo muhimu kwao.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.