WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI WAASWA KUFANYA KAZI KWA BIDII
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe,Rukia Muwango amewaasa Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji kufanya kazi kwa bidii ili kufikisha huduma inayostahili kwa jamii na kuondoa manung’uniko miongoni mwa jamii.
Amesema hayo hivi karibuni katika kikao cha kazi kilicholenga kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwao na pia kuwapa maelekezo mbalimbali ya Serikali.
Katika maelekezo yake aliwataka watendaji hao kutekeleza shughuli mbalimbali za serikali kwa ari na weledi ikiwemo suala la usafi wa mazingira,kujiwekea maelengo na mpango wa kazi katika shughuli zao ili ziweze kuwa na tija.
“Simamieni zoezi la usafi wa mazingira katika kata zenu na vijiji,suala la kuondoa utoro kwenye shule zilizopo katika maeneo yenu”Aliongeza Mhe Muwango.
Aidha amewataka kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kutoa taarifa pale wanapoona mtu wanayemtilia shaka katika maeneo yao,hii ikiwa ni pamoja wanyeviti wa vitongoji kufuatilia wageni wanaoingia maeneo yao na kujiridhisha ukaazi wao kupitia vitambulisho vyao.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.