Wananchi watakiwa kutunza mazingira
Wananchi wamehamasishwa kutunza mazingira kwa kufanya usafi katika maeneo yao ili kuepuka magonjwa yanayoweza kusasababishwa na uchafuzi wa mazingira.
Hayo yamesemwa jana na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Nachingwea Mheshimiwa Mustafa Mmuni katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyofanyika kiwilaya katika viwanja vya dampo la uhindini kata ya Nachingwea.
“Kila mtu katika eneo lake ajitahidi kufanya usafi, wenyeviti wa vitongoji tengenezeni utaratibu wa kuwabaini watu wote wanaotupa taka hovyo na matairi kwenye dampo ili kuweza kuwashughulikia” Alisema Mheshimiwa Mmuni
Aidha Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Nachingwea Arbogast Kiwale amewataka wakazi wa Mji mdogo wa Nachingwea kushirikiana na Serikali kuhakikisha mji unakuwa safi.
Katika maadhimisho hayo wananchi wamejitokeza kwa wingi kufanya usafi katika dampo la uhindi na meneo yanayolizunguka, kauli mbiu ya siku ya mazingira mwaka huu “mkaa ni gharama,tumia nishati mmbadala”
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.