Taasisi ya UNWomen wakishirikiana na Halmashauri ya Nachingwea wameendelea kutoa mafunzo kwa wanawake, June 30, 2024 wametembelea Shule ya Sekondari ya farm 17 pamoja na sekondari ya Kipaumbele kuzungumza na wanafunzi wakike juu ya kujitambua wao katika nafasi zao pamoja na kuwafundisha stadi za maisha.
Afisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri amewasihi wanafnzi hao kutoruka hatua katika kukua kwao na badala yake amewataka kuzingatia elimu na kujenga uwezo wakujiamini na kutokubali mtu kuwaingilia katikati.
Aidha, wanafunzi hao wamesisitizwa kuzishika stadi za maisha pale wanapofundishwa kujitegemea na kufanya kazi nyumbani au shuleni wasiwe wategevu kwani itawajenga na kuwasaidia katika maisha yao, pia wametakiwa kutofanya vitendo vya uyanyapaa ni vibaya na vinachangia maambukizi mapya ya ukimwi "tuache unyanyapaa", mwisho amewasihi wanafunzi wajitunze na wale wenye mambukizi wasiambukize wenzao.
#wizarayamaendeleoyajamiiwanawakenawatoto
#unwomen
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.