Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Hashim Komba amewataka viongozi waliogawana fedha za Kijiji cha Kiegei A kurejesha fedha hizo mara moja
Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo jana kwenye mkutano wa kusikiliza kero uliofanyika katika Kijiji cha Kiegei B katikati janai baada ya kupokea kero ya matumizi mabaya ya fedha za Kijiji kutoka kwa wananchi.
Alimtaka Afisa Tarafa na Afisa Kilimo kusimamia fedha hizo zirejeshwe mpaka kufikia siku ya Ijumaa saa 10:00 Jioni kwa kuwatafuta wajumbe wote wa Serikali waliohusika katika mgao huo wa fedha.
“Haiwezekani choo hakijaisha, wajumbe na Mtendaji wa Kijiji wanagawana fedha za wananchi shilingi laki saba kwa kisingizio eti wajumbe wamemaliza muda wao” Alisema Mheshimiwa Komba
Mkuu wa Wilaya alimuagiza Kamanda wa Polisi Wilaya kuwakamata watu wote ambao hadi kufikia muda aliouweka watakuwa hawajaresha fedha hizo washikiliwe mpaka pale fedha hizo zitakaporejeshwa.
Pia amewaasa watumishi wa umma kufanya kazi kwa uadilifu na uzalendo mkubwa kwa kufanya matumizi sahihi ya fedha zinazoletwa kukamilisha miradi ya Maendeleo.
Katika mkutano huo wananchi ishirini walijitokeza kueleza kero zao ambazo baadhi yake zilipatiwa majawabu na wataalam walioongozana na Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.