Vijana watahadharishwa kujihadhari na wanafunzi
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amewatahadharisha vijana kuhusu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi kuwa ni hatari sana.
Ametoa tahadhari hiyo jana wakati akiongea na wananchi Kijiji cha Kilimarondo, Kata ya Kilimarondo tarafa ya Kilimarondo alipokuwa akifanya mkutano wa hadhara baada ya kukagua kituo cha afya Kilimarondo.
“Ukimchezea mwanafunzi ujiandae kufungwa, serikali haina mzaha kwa mtu yeyote atakayemtia mimba mwanafunzi kuna tabia ya bodaboda kuwahadaa wanafunzi jihadharini mtafungwa” Amesema mheshimiwa Majaliwa.
Aidha Mheshimiwa Waziri Mkuu amekabidhi saruji tani mbili na nusu kwa uongozi wa kijiji cha Mpiruka A ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa alipofanya alipoongea na wanakijiji cha Mpiruka mapema mwaka huu.
Waziri Mkuu amefanya ziara ya siku moja katika Wilaya ya Nachingwea kwa mwaliko wa Mheshimiwa Mbunge ambapo amesikiliza kero za wananchi wa kata za Namatula, Mtua , Mbondo na Kilimarondo.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.