Mkuu wa wa Wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo amewasihi wakazi wa Wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha pale zoezi hilo litakapoanza tarehe 11 - 20 mwezi wa 10, 2024 na kujitokeza kupiga kura kwa wingi siku ya tarehe 27, Mwezi wa 10, 2024.
Hayo ameyasema Oktoba 5, 2024 alipokua katika Bonanza la Nachingwea ya Amani na Maendeleo lilioandaliwa na Msimamizi wa Uchaguzi kwa ajili ya kuhamasisha masuala la amani, kuonesha maendeleo yaliyofanywa na Serikali na kuhamasisha wananchi kushiriki Uchaguzi wa serikali za mitaa.
Bonanza ambalo limekwenda sambamba na Kauli mbiu isemayo "Nachingwea ya Amani na Maendeleo,Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi".
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.